Home Dauda TV KAMA ULIPITWA NA GOLI LA ‘KIDEONI’ LA AJIB, MZIGO WOTE UPO DAUDA...

KAMA ULIPITWA NA GOLI LA ‘KIDEONI’ LA AJIB, MZIGO WOTE UPO DAUDA TV

919
0
SHARE

Ajib-goal

February 3, 2016 ligi ya Vodacom Tanzania bara iliendelea kwenye viwanja kadhaa ya miji tofauti ya Tanzania, uwanja wa taifa Simba ilitoa kipondo cha bao 5-1 dhidi ya Mgambo JKT ya moani Tanga.

Wachezaji wa Simba waliopeleka mvua ya magoli kwa wanajeshi hao wa Handeni ni Hamisi Kiiza aliyetupia bao mbili kambani halafu Daniel Lyanga, Ibrahim Ajib na Mwinyi Kazimoto wakafunga goli moja kila mmoja.

Goli ambalo lilikuwa kivutio kwa wapenzi wa Simba ni lile lililofungwa na nyota wa Simba Ibrahim Ajib aliyeivuruga safu ya ulinzi ya Mgambo kisha kufunga bao lake kwa ustadi mkubwa.

Kama ulipitwa na uhondo huo, Dauda TV inakupa fursa ya kushuhudia mautundu ya mtoto Ajib kwenye video hapa chini.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here