Home Ligi EPL MAMBO 5 YANAYOTARAJIWA MANCHESTER CITY CHINI YA UTAWALA WA GUARDIOLA 

MAMBO 5 YANAYOTARAJIWA MANCHESTER CITY CHINI YA UTAWALA WA GUARDIOLA 

2117
0
SHARE

Guadiola-Man C

Uhamisho wa Guardiola kuelekea Manchester City ilikuwa ni moja kati ya siri kubwa huku
akihusishwa kujiunga Manchester united lakini sasa imekuwa wazi kuwa atajiunga Manchester
City mwishoni mwa msimu. Kocha huyo takribani kila timu anayoifundisha hutwaa mataji,
amefanya hivyo akiwa na Barcelona sasa Bayern Munich. Je tutarajie nini kwa mwaka 2016/2017?

  1. KUHAMA KWA NGUVU YA UTAWALA EPL

Manchester City wameshinda mataji mawili ya ligi kuu kwa siku za karibuni, Huku wakiwa
wamewekeza mamilioni na millioni katika kusajili wachezaji wa dunia kwa lengo la kuleta
mafanikio. Lakini haikuweza kuwa dawa ya wao kuweza kupata mafanikio chini ya Mancini na sasa. Pellegrin japokuwa wametwaa ubingwa mara 2 lakini kutokana na vipaji walivyonavyo
inaonesha wamefeli. Katika EPL kuna kitu kinaitwa “kelele za majirani” na sasa Manchester City wapo katika michuano yote. Kiongozi wa viongozi, Guardiloa kafika huenda upepo ukabadilika.

  1. KUNUFAIKA KWA ACADEMY ZA VIJANA ZA MANCHESTER CITY

Akademi ya Manchester city ipo polepole japo ni nembo.viongozi wa Manchester City
wamejaribu kuwekeza katika miundombinu na kuleta makocha lakini hali halisi inaonekana.
Kituo hicho kimetoa vijana wengi chini ya umri wa miaka 16 na 21 kuliko Manchester United, Arsenal na Liverpool. Je watashindwaje kufanikiwa endapo Guardiola atahamishia nguvu zake pale? Miundombinu ipo tayari katika timu inahitaji kiongozi wa kuongoza. Falsafa za kocha huyo ya kumiliki mpira, kucheza kuanzia nyuma na uwezo wa kulinda inajulikana kwa wote lakini kuwa-manage wachezaji wote sio rahisi ataweka uelewa wake na mbinu ambapo ni muhimu kuwakuza wachezaji watakaoendana na mfumo wake. Muulize Sergio Bosquets na Pedro.

  1. KUONDOKA KWA BAADHI YA WACHEZAJI

Wakati mashabiki wa Manchester City wakifurahia ujio wa Guardiola kuna baadhi ya wachezaji hawajapendwa kufundishwa na kocha huyo mmoja wao ni Yaya Toure. Kauli ya wakala wa Yaya inaongeza chachu ya kuondoka kwa Yaya Manchester City.  Dimitri Seluk mwezi uliopita alimponda Giardiola kwa kusema “ukweli ni kwamba hata babu yangu angeshinda vikombe endapo angezifundisha Barcelona na Bayern munich kutokana na kuwa ni timu kubwa zenye wachezaji wakubwa”.

Toure hata kuwa chaguo la Guardiola ambapo hakuaminiwa Barcelona ndipo Guardiola alimuamini Bosquets katika majukumu ya kiungo wa kati. Wakati wa Toure umefika ukingoni kwa sasa.

  1. UJIO WA WACHEZAJI WAPYA

Ujio wa wachezaji wapya itakuwa gumzo kwa City. Viongozi wa Manchester City wanefurahia kumuona pep City kwanini wasitue wachezaji wapya Etihad? Lewandowiski hatua yake imekuwa sitofahamu akitajwa kuchukua nafasi ya Bonny. Thiago Alcantara alimfuata Ujerumani Guardiola na itakuwa salama endapo atapenda kucheza chini ya Guardiola.

  1. LIGI YA MABINGWA ULAYA

Ingawa Manchester City wamewekeza kwenye EPL hali ni tofauti kwenye ligi ya mabingwa
wakati klabu za England zinafanya vibaya. Manchester United, Chelsea na Liverpool
walishinda taji hilo muongo uliopita. Mfumo utabadilika kulingana na ugumu wa mchezo ulinzi na matokeo ni muhimu zaidi kupata mafanikio kwenye ligi ya mabingwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here