Home Ligi EPL Wenger: Sitosajili mchezaji yoyote leo labda nipewe nafasi ya kumsajili Messi Tu.

Wenger: Sitosajili mchezaji yoyote leo labda nipewe nafasi ya kumsajili Messi Tu.

652
0
SHARE

Dirisha la usajili barani ulaya linafungwa leo usiku 5.59 kwa saa za Afrika Mashariki, mashabiki wa vilabu mbalimbali wakifuatilia kwa karibu kuona timu zao zitafanya usajili wa kujiimarisha – mojawapo ya vilabu hivyo ni klabu ya Arsenal, ambayo kocha wake Arsene Wenger amesema kwamba ana uhakika wa asilimia “99” kwamba hatosajili mchezaji yoyote isipokuwa ikitokea mchezaji tu akiwa sokoni.IMG_3087.JPG

Wenger amesema iwapo tu Lionel Messi atakuwa anauzwa ndio washabiki wa klabu yake wategemee kuiona Arsenal ikisajili mchezaji siku ya leo.

Gunners tayari wameshamsajili kiungo Mohamed Elneny katika dirisha hili la usajili – usajili ambao washabiki wengi wanaona bado hautoshelezi mahitaji ya klabu katika mapambano ya mbio za ubingwa wa EPL.

“Dirisha hili la usajili limekuwa la ukimya mno tofauti na mategemeo yangu. Mimi ni mmoja wa wachache tuliofanya biashara kwenye dirisha hili. Niliwaambia tutafanya angalau usajili wa mchezaji mmoja, ningependa kufanya biashara zaidi katika dirisha hili lakini ukosefu wa wachezaji wanaokidhi mahitaji yangu katika soko umesababisha ukimya huu kwenye dirisha hili la usajili.

“Lolote linaweza kuwa kutokea, lakini nina uhakika asilimia 99 kwamba hakutakuwa na usajili mwingine, labda itokee nafasi ya kumsajili Messi – sitomwambia tafadhali rejea Barcelona.’ Arsenal-v-West-Ham-United-Premier-League

Wenger pia amethibitisha kwamba Mathieu Debuchy na Serge Gnabry wote wanaweza kuondoka kwa mikopo – huku DEBUCHY akiwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kubaki katika ligi kuu ya England na Gnabry akiwa na uwezekano wa kwenda  Championship.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here