Home Kitaifa DAR SWIM CLUB YASHINDA MASHINANO YA KUOGELEA TALISS

DAR SWIM CLUB YASHINDA MASHINANO YA KUOGELEA TALISS

818
0
SHARE
Waogeleaji waki -dive kwenye maji katika mashindano hayo
Waogeleaji waki -dive kwenye maji katika mashindano hayo
Waogeleaji waki -dive kwenye maji katika mashindano hayo

Na Mwandishi wetu

Timu ya Dar Swim Club (DSC) imeshinda mashindano ya kuogelea ya Taliss baada ya kuzipiku klabu nyingine nane zilizoshiriki katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Upanga.

Dar Swim Club  ilijikusanyia pointi 2,421 katika mashindano hayo yaliyoshirikisha timu za wanawake na wanaume. Katika mashindano hayo, wanawake wa DSC walikusanya jumla ya pointi 1,526 huku wanaume wakijikusanyia pointu 895 kushinda nafasi ya kwanza katika mashindano hayo yaliyokuwa na ushindani mkubwa.

waogeaji wakichuana katika mashindano hayo
waogeaji wakichuana katika mashindano hayo

Waogeleaji wa kike Smriti Gokarn, Celina Itatiro na Maia Tumiotto walichangia zaidi ushindi wa timu hiyo kwa kukusanya pointi nyingi na kwa upande wa wavulana walikuwa Matt Golembeski, Marin De Villard na Carter Golembeski.

Nafasi ya pili imenyakuliwa na wenyeji Taliss kwa kupata jumla ya pointi 2,298 huu waogelaji wao wa kiume, Adil Dharmal na  Oliver Mclntosh wakiongoza kwa kuchangia pointi nyingi katika ushindi huo.

Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Shule ya Kimataifa ya Moshi ambayo ilichanganyika na ya Arusha kwa kupata pointi 1,111 huku waogeleaji wake, Josephine Oosterhuis na Pieter De Raadt wakichangia pointi nyingi.

Wachezaji na makocha wa timu ya Dar Swim Club wakishangilia baada ya kutwa ushindi wa jumla katika mashindani ya Taliss yaliyofanyika jana kwenye bwawa la kuogelea la shule ya kimataifa ya Tangangika (IST Upanga) na kushirikisha jumla ya timu tisa
Wachezaji na makocha wa timu ya Dar Swim Club wakishangilia baada ya kutwa ushindi wa jumla katika mashindani ya Taliss yaliyofanyika jana kwenye bwawa la kuogelea la shule ya kimataifa ya Tangangika (IST Upanga) na kushirikisha jumla ya timu tisa

Timu ya kuoglea ya Mwanza ilimaliza katika nafasi ya nne chini ya waogeleaji nyota Elia Imhoff na Emma Imhoff  na kufuatiwa ma shule ya kimataifa ya Morogoro chini ya nyota wake, Dennis Mhini na Charlotte Sanford.

Timu ya Bluefins ilishika nafasi ya sita kwa pointi  553 ambapo waogelaji wake Sahal Harunani alishinda medali ya shaba. Nafasi ya saba ilikwenda kwa timu ya Wahoo iliyokuwa chini ya Ellis Underson na Rania Karume kwa kupata pointi 303 na  huku Champions Rise na Kennedy House wakimaliza katika nafasi mbili za mwisho.

Muasisi wa Dar Swim Club Ferick Kalengela alisema kuwa siri kubwa ya ushindi wao ni kujituma na kufanya mazoezi ya kisasa huku Katibu mkuu wa klabu hiyo, Inviolata Itatiro akiwapongeza wachezaji wake na kusema huo ni mwanzo tu na makubwa yatafuatia katika kuendeleza mchezo wa kuogelea nchini.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here