Home Kimataifa ULIMWENGU: SIKU SI NYINGI NA MIMI NAMFUTA NYUMA SAMATTA

ULIMWENGU: SIKU SI NYINGI NA MIMI NAMFUTA NYUMA SAMATTA

897
0
SHARE

Samatta Ulimwengu 1

Thomas Ulimwengu ni mchezaji ambaye amecheza kwa muda mrefu na Mbwana Samatta kwenye klabu ya TP Mazembe. Samatta ameshatambulishwa kwenye klabu ya Genk na wamechana rasmi na rafiki yake kipenzi ‘pacha’ Ulimwenu, shaffihdauda.co.tz imepiga story na Ulimwengu kutaka kujua mambo kadhaa kuhusu kuondoka kwa Samatta nay eye ataathirika vipi kutokana na kuodoka kwake.

Jambo zuri ni kwamba, Ulimengu ameihakikishia shaffihdauda.co.tz siku si nyingi huenda nay eye akaihama klabu ya TP Mazembe na kwenda kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Shaffihdauda.co.tz: Mbwana Samatta amesajiliwa rasmi na Genk nini maoni yako juu ya usajili wake?

Ulimwengu: Mimi kwangu ni furaha kubwa sana, kama nilivyosema mwanzo Samatta ameshafungua njia kwa watanzania wote wachezaji mpira wajue kabisa njia imeshafunguliwa kwahiyo ma-agent wengi watakuwa wanaangalia Tanzania kwahiyo tutumie fursa hiyo.

Shaffihdauda.co.tz: Wew binafsi kubaki katika klabu ya TP Mazembe bila ya uwepo wa Mbwana Samatta itakuathiri kisaikolojia kwa kiasi gani?

Ulimwengu: Nitamkumbuka kama rafiki yangu tulikuwa tunaishi pamoja kikubwa ndiyo hicho. Lakinin katikati ya uwanja haitaniathiri sana uwezo wangu ila tuta-miss uwepo wake pale mbele.

Shaffihdauda.co.tz: Mashabiki wa TP Mazembe wanazungumziaje kuondoka kwa Mbwana Samatta?

Ulimwengu: Mashabiki wanalia sana lakini wengi wanamtakia mafanikio mema, watamkumbuka sana. Siyo mashabiki tu hata sisi wachezaji tutamkumbuka

Shaffihdauda.co.tz: Tukutarajie na wewe siku za karibuni kuihama Mazembe na kwenda kwenye vilabu vya Ulaya au bado upo Mazembe kwa muda?

Ulimwengu: Tuombe uzima tu, siku si nyingi na mimi namfuta nyuma.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here