Home Kimataifa Alichokisema Waziri Nape Nnauye baada ya Mbwana Samatta kusajiliwa Genk

Alichokisema Waziri Nape Nnauye baada ya Mbwana Samatta kusajiliwa Genk

752
0
SHARE


Screen Shot 2016-01-30 at 2.46.26 PM

Jana habari kubwa kwa wapenda soka wote ilikua ni kuhusu mtanzania Mbwana Samatta kujiunga na club ya KRC Genk akitokea TP Mazembe. Mbwana amekua mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kujiunga na club hii ambayo inashiriki ligi kuu ya Ubeligiji.

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye alikua bega kwa bega na Mbwana Samatta kabla na baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Africa kwenye CAF Glo Awards.

Baada ya jana habari za Samatta kusajiliwa na Genk kumfikia,Nape Nnauye ametumia page yake ya twitter kuandika Serikali tulipoamua kumsaidia, tulisemwa tumeanza udalali, leo matunda ya “udalali” haya hapa! ”.

Serikali imempa support Mbwana Samatta hata kabla hajawa mchezaji bora wa Africa tangu alivyokua Congo ambapo Rais Jakaya Kikwete alienda kumtembelea alivyokua ziarani na kuongea nae maneno ambayo Samatta anasema yaliwatia moyo yeye na mwenzake Ulimwengu.

Screen Shot 2016-01-30 at 2.45.18 PM

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here