Home Kimataifa SAMATTA KUFUATA NYAYO ZA BENTEKE, DE BRUYNE NA COURTOIS? USOME WASIFU WA...

SAMATTA KUFUATA NYAYO ZA BENTEKE, DE BRUYNE NA COURTOIS? USOME WASIFU WA KLABU YAKE MPYA

966
0
SHARE

Sakata la usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta kwenda kucheza soka barani ulaya hatimaye limemalizika leo hii baada ya kusaini mkataba wa miaka 4 na klabu ya Koninklijke Racing Club Genk.

IMG-20160129-WA0006 KRC Genk ni moja ya klabu kongwe na kubwa sana nchini Belgium ambayo inashiriki katika ligi kuu ya nchi hiyo na tayari imeshashinda vikombe vitatu vya ligi hiyo katika misimu ya 1998–99, in 2001–02 and in 2010–11.

30
Thibaut Courtois alipokuwa Genk

Klabu hiyo ambayo makazi yake yapo katika jiji la Genk huko katika eneo la Belgian Limburg pia imewahi kushinda vikombe vya FA vinne, mara ya mwisho ilikuwa katika misimu ya 2008–09 and in 2012–13. Genk pia imekuwa ikishiriki kwenye michuano mikubwa zaidi barani ulaya katika ngazi ya vilabu –  UEFA Champions League ambapo katika misimu ya  2002–03 and 2011–12 waliishia hatua ya makundi.

Kevin De Bruyne alipokuwa akiichezea KRC Genk
Kevin De Bruyne alipokuwa akiichezea KRC Genk

Klabu hii ilianzishwa mwaka 1988 kwa kuviunganisha vilabu vya Waterschei Thor na KFC Winterslag. Klabu hii imekuwa moja ya vilabu vilivyofanikiwa sana nchini Belgium tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990 na wamekuwa wakishiriki mara kwa mara kwenye michuano ya ulaya. Klabu hii imekuwa ikicheza kwenye ligi kuu ya Belgium tangu msimu wa 1996–97 season. Huwa wanautumia uwanja wa Cristal Arena kama dimba lao la kuchezea mechi za nyumbani. Wanatumia jezi za Blue na Nyeupe.

Christian+Benteke+KRC+Genk+vs+KAA+Gent+Jupiler+8qcZWXC8-Myl
Christian Benteke kabla ya kuuzwa kwenda Aston Villa

Genk imekuwa ni moja ya klabu za Belgium zinazosifika kwa kuwafungulia milango wachezaji wengi kwenda kwenye timu kubwa barani ulaya, baadhi ya wachezaji ambao wameshawahi kupita Genk na kuuzwa kwenda vilabu vikubwa ni Davick Origi – Liverpool Christian Benteke – Aston Villa na sasa Liverpool, Kevin De Bruyne na Thibaut Courtois kwenda Chelsea mwaka 2012.

KRC Genk ni moja ya vilabu vilivyo na sifa ya kukuza na kuvilisha vilabu vikubwa ambavyo vina makubaliano nao ya kibiashara ya kuuziana wachezaji kutoka kwenye timu yao na academy.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here