Home Ligi EPL WENGER AMUANGUSHIA DIEGO COSTA ZIGO LA LAWAMA

WENGER AMUANGUSHIA DIEGO COSTA ZIGO LA LAWAMA

616
0
SHARE

Costa Diego 1

Baada ya kipigo cha bao 1-0 wakiwa katika uwanja wao wa Emirates, toka kwa klabu ya Chelsea, kocha wa Arsenal mfaransa Arsene Wenger amesema pamoja na kuwa mlinzi wake wa kati Per Mertesacker kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo huo, lakini akamtupia lawama mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa kuwa ndiye alikua sababu.

Per Mertesacker alioneshwa kadi nyekundu katika dakika ya 18 ya mchezo huo baada ya kumzuia nafasi ya kufunga goli mshambuliaji Diego Costa wa Chelsea kwa kumchezea rafu kwa nyuma.

Lakini kocha Arsene Wenger akimtetea mchezaji wake amesema ni halali kwa Mertesacker kuoneshwa kadi nyekundu lakini akasema kuwa ni ujanja wa mshambuliaji Diego Costa kumsababishia kadi hiyo mlinzi wake wa kati.

“Alisababisha Paulista apewe kadi nyekundu katika mchezo wetu wa kwanza, na sasa anamsababishia Mertesacker naye atolewe nje kwa kadi nyekundu, hivyo ni ujanja mkubwa”, alisema Arsene Wenger.

Wachezaji wa nne wa Arsenal tayari wamekwisha tolewa nje kwa kadi nyekundu katika michezo mitano iliyopita dhidi ya Chelsea, ni mzimu mbaya kwa vijana hao wa Arsene Wenger dhidi ya Chelsea.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here