Home Entertainment Baada ya Mtoto wa Jorge Mendes – Ronaldo sasa Ahusishwa kutoka na...

Baada ya Mtoto wa Jorge Mendes – Ronaldo sasa Ahusishwa kutoka na Mdogo wake Kim Kardashian

1236
0
SHARE

Takribani mwaka mmoja tangu kuachana na girlfriend wake, mwanamitindo wa kirusi Irina Shayk – Cristiano Ronaldo ameendelea kuhusishwa na mahusiano na wasichana mbalimbali duniani.

 
Baada ya kuhusishwa na mtoto wa wakala wake Jorge Mendes miezi kadhaa iliyopita, hivi sasa CR7 ameanza kuhusishwa na mdogo wake Kim Kardashian – aitwaye Kendall Jenner. 

 Mshambuliaji huyo Real Madrid, 30, hivi karibuni amekuwa akionyesha kuvutiwa sana na Kendall ambaye pia ni mwanamitindo maarufu kama ilivyokuwa kwa Irina. 

Ronaldo amekuwa aki-like picha nyingi za Kendall katika mtandao wa Instagram – na mapema leo shabiki mmoja raia wa Croatia alibahatika kuona akaunti ya Ronaldo iki-like picha ya Kendall na akai-screenshot. 

Na hii sio mara ya kwanza kwa Ronaldo kuonekana akimmendea Kendall on Instagram kwa kuifuatilia akaunti ya mwanadada huyo na kuonyesha anavyovutiwa na binti huyo mwenye followers millioni 40 katika mtandao huo wa kijamii.


Gazeti la The Sun linaelezea kwamba Kendall, 20, anafurahishwa sana na attention anayopewa na Ronaldo, kwa mujibu wa marafiki zake wa karibu walioripotiwa na mtandao wa HollywoodLife. 

  
Kendall Jenner, ni mdogo wa pili wa mke wa rapa Kanye West, Kim Kardashian ambaye nae aliwahi kuhusishwa kutoka kimapenzi na Ronaldo wakati alipokuwa anaitumikia Manchester United. 
 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here