Home Ligi BUNDESLIGA BUNDESLIGA IMEREJEA, LEWANDOWSKI AFANYA YAKE

BUNDESLIGA IMEREJEA, LEWANDOWSKI AFANYA YAKE

627
0
SHARE

Lewandowski 1

Usiku wa January 22, 2016 ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga iliendelea baada ya mapumziko mafupi ya kipindi cha baridi, habari kubwa kwenye ligi hiyo ni ushindi wa Bayern Munich wa magoli 2-1 dhidi ya Hamburg.

Robert Lewandowski alitupia bao zote mbili kwenye mchezo huo ambao umeishuhudia Bayern ikiendelea kupaa kileleni mwa ligi hiyo kwa tofauti ya ponti 11 kwa timu iyoifuatia.

Lewandowski 2

Lewandowski alianza kupachika bao la kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya Thomas Muller kuangushwa kwenye eneo la hatari na golikipa wa Hamburg Rene Adler.

Hamburg walisawazisha kwa bao la kujifunga la Xabi Alonso wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa free-kick ya Aaron Hunt.

Lewandowski 4

Lakini Lewandowski aliihakikishia the Bavarians ushindi baada ya kupachika bao la pili kwenye mchezo huo.

Lewandowski 3

Mabao hayo yanamfanya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Poland kubakiza goli moja ili kumfikia kinara wa kupachika mabao kwenye ligi hiyo ambaye ni striker wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang mwenye magoli 17 hadi sasa.

Lewandowski 2

Free-kick ya David Alaba iligonga mwamba wakati kocha wa Bayern Pep Guardiola alimshuhudia beki wake Jerome Boateng akilazimika kwenda nje ya uwanja kutokana na majeruhi.

Guardiola-Bayern

Huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza wa kimashindano tangu Guardiola atangaze kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu na kutimkia England.

Bayern-Msimamo

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here