Home Entertainment Mesut Ozil amesema kama angekua msanii wa Hiphop angefanya collabo na huyu.

Mesut Ozil amesema kama angekua msanii wa Hiphop angefanya collabo na huyu.

713
0
SHARE

ozil

Mesut Ozil kama wachezaji wengine anapenda kusikiliza muziki kabla na baada ya mechi. Sasa akiwa kwenye moja ya interview alizungumzia kuhusu ishu ya yeye kuwa mpenzi mkubwa wa muziki hasa wa Hiphop.

“Nasikiliza muziki kabla ya mechi na baada ya mechi wakati wote ili kujipa hype au kutulia baada ya mechi. Mimi ni mtu wa Hiphop sana na sasa hivi sio rahisi kusema msanii gani yupo juu kwenye game ya HiHop. Napenda kila kitu kwenye Hiphop kuanzia mashairi hadi style ya ku-perfom.”

Ozil alienda mbali hadi kuzungumzia ishu ya yeye kama angeweza kuingia studio basi anapenda kufanya kazi na msanii gani. “Kama ningepata nafasi ya kuingia studio na msanii wa Hiphop muda wowote ningemchagua Kanye West.Kanye ndio msanii wangu ambae namkubali sana, baada ya Kanye wanafuatia Wiz Khalifa then anakuja Drake.”

Bingwa assist hivi ingekuaje anaingia studio na kutoa kitu na Kanye West. Kwenye kikosi cha Arsenal kipa wao Cech ni mkali wa kupiga drums na Sanchez ni mkali wa kupiga keyboard. Wakiingia studio wanaweza kutoa ngoma.

sdfddhdf hgg

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here