Home Kimataifa BBC vs MSN: Nani Kiboko ya Magoli Msimu Huu – Wote Pamoja...

BBC vs MSN: Nani Kiboko ya Magoli Msimu Huu – Wote Pamoja Wavuja Rekodi Hii

771
0
SHARE

Pea mbili za ‘Utatu mtakatifu’ unaoundwa na washambuliaji sita wa vilabu vya Real Madrid na FC Barcelona – BBC na MSN zimeendelea kuweka rekodi mpya za ufungaji wa magoli barani ulaya.

14530745382038Safu mbili za ushambuliaji zilizo hatari zaidi katika ulimwengu wa soka hivi sasa, zimeshafunga magoli 89 kwa pamoja: BBC inayoundwa na Benzema, Bale na Cristiano Ronaldo wamefunga jumla ya magoli 45 na MSN inayoundwa na Messi, Suarez na Neymar wamefunga magoli 44. Kwa pea hizi mbili mara zote kunakuwaga na rekodi za kuvunja na jumapili iliyopita kwa mara ya kwanza kabisa wote sita walifunga katika raundi moja ya mechi za La Liga.

Mpaka kufikia sasa, ilikuwa ni kwenye raundi ya 13 ambapo wengi wao walifunga katika mechi za timu zao, ilikuwa ni Karim Benzema tu aliyeshindwa kufunga dhidi ya Eibar.

Kwa upande wa BBC, hii ilikuwa ni mara yao ya 7 kwa wao wote kufunga, mara ya 3 ya wote kufunga msimu huu, kwa MSN – hii ilikuwa mara yao ya pili kufunga wote msimu huu, mara ya kwanza walifunga mabao manne katika mechi ya Real Sociedad katika raundi ya 13.

Kwa Barcelona, angalau mchezaji mmoja amefunga katika mechi 17 kati ya 20 zilizopita, wakati BBC walikuwa na michezo mitano ambayo hawakufunga kabisa.

Magoli 10 yaliyofungwa na MSN na BBC ndio rekodi yao kubwa kabisa – rekodi yao kubwa ilikuwa magoli 9 ambayo walifunga katika raundi ya 16 na 19.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here