Home Ligi EPL Mkosi wa Stoke City: Man UTD na City Zisahau Ubingwa, Arsena au...

Mkosi wa Stoke City: Man UTD na City Zisahau Ubingwa, Arsena au Leceister Kutwaa Ubingwa wa EPL

1558
0
SHARE

Vilabu vya ARSENAL, Leicester au Tottenham – moja ya kati ya vilabu hivi inaweza kuwa bingwa wa ligi kuu ya England kama historia itakuwa ina namna ya kujirudia. 01_18100749_76d213_2645862aTangu Stoke City walipowasili kwenye EPL msimu wa 2008/08, hakuna timu ambayo ambayo waliifunga katika uwanja wao wa Britannia halafu timu hiyo ikaenda kutwaa ubingwa wa EPL msimu huo.

Mpaka sasa ni timu mbili tu za juu ambazo zilitoka katika dimba la Britanna bila kufungwa nazo ni Arsenal na Leceister, huku vigogo wa jiji la Manchester – United na City wenyewe walipokea vipigo kutoka kwa Stoke katika dimba la Britannia.

Historia inatuambia kwamba kutokana na rekodi hizo hapo juu – vijana wa Arsene Wenger na Claudio Ranieri ndio wanaoweza kutwaa ubingwa wa EPL kufikia May 2016.

Mkosi wa kufungwa Britannia unaweza kuwakumba Manuel Pellegrini na Louis van Gaal ambao walipoteza mechi katika uwanja huo kwa kupokea vipigo vya 2-0 kila mmoja – msimu huu.

Moja ya timu ambazo zinatajwa kugombea ubingwa safari hii, Tottenham – wao pekee ndio bado hawajacheza na Stoke katika dimba la Britannia.

Hivyo kama mkosi huu wa dimba la Britannia utaendelea kuwepo, basi Spurs itabidi wajitahidi kupata matokeo chanya wakati watakapoenda kupambana na Stoke mnamo April 16 – ili waweze kujiweka mahala pazuri kwenye safari yao ya kupata ubingwa wa kwanza wa ligi tangu mwaka 1961.

STOKE_Cup_table_2645960aStoke walipopanda daraja msimu wa 2008/09 РManchester United waliwafunga  1-0 @Britannia kisha wakaenda kutwaa ubingwa wa msimu huo.

Msimu uliofuatia – mabingwa walikuwa Chelsea na walipata matokeo ya 2-1 dhidi ya Stoke @Britannia – United walipochukua ubingwa msimu wa 2010/11 waliwafunga 2-1.

City walipata sare ya 1-1 dhidi ya Stoke @Britannia katika msimu waliochukua ubingwa wao wa kwanza wa EPL mwaka 2012, na msimu uliofuatia United wakashinda 2-0.

History ilijirudia tena misimu miwili iliyopita wakati City walipopata sare tasa @Britannia na wakaenda kutwaa ubingwa, kabla ya Chelsea kurudi London na ushindi wa 2-0 kabla ya kwenda kutwaa ubingwa msimu uliopita.

Seasons-results-ta_2645968aMsimu huu Leicester wamepata sare ya 2-2 na jana usiku Gunners wakapata sare ya 0-0 – hivyo mpaka sasa ni vilabu hivyo tu ambavyo vimepata matokeo chanya katika dimba la Britannia.

Kwa wale wazee wa KuBET – mnaweza kuanza kuwawekea mizigo Leceister, Arsenal na labda Tottenham kwamba wanaweza kutwaa ubingwa wa EPL.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here