Home Kimataifa AC Milan inampeleka mchezaji huyu mahakamani kwa kuwaongopea umri.

AC Milan inampeleka mchezaji huyu mahakamani kwa kuwaongopea umri.

635
0
SHARE

sha31

Wachezaji wa Africa mara nyingi huwa wanajikuta kwenye tatizo la kudanganya umri wakiwa wanataka kucheza Ulaya.

Yusupha Yaffa ni mchezaji wa Gambia ambae alifanikiwa kuiongopea club kubwa AC Milan kwamba ana miaka 19 wakati ana miaka 28. Mchezaji huyu alifanikiwa kuingia kwenye mpango wa timu ya vijana na kucheza kwenye kikosi cha u19 baada ya viongozi wa club hiyo kukubali ana miaka 19.

Taarifa za mchezaji huyu kugundulika kwamba ana miaka 28 na sio 19 ilianzia kwenye Facebook ambapo rafiki yake aliweka post ambayo inaelezea ishu hiyo.

Sasa hivi mchezaji huyu anacheza nchini Ujerumani club ya MSV Duisburg na huko pia inasemekana  mkataba unakaribia kuvunjwa kwasababu ya ishu hii.

AC Milan imefungua mashtaka ndani ya mahakama ya Italy dhidi ya mchezaji huyu. Hii sio mara ya kwanza kwa Yaffa kufikishwa mahakamani, aliwahi kuwa na kesi ya kumbaka binti mmoja huko Ujerumani.

sha1

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here