Home Ligi EPL Hivi ni vitu usivyovijua kuhusu mchezaji mpya wa Arsenal Mohamed Elneny

Hivi ni vitu usivyovijua kuhusu mchezaji mpya wa Arsenal Mohamed Elneny

763
0
SHARE

Screen Shot 2016-01-14 at 9.29.10 PM

Hivi sasa umetangazwa usajili mpya wa mchezaji raia wa Egypt Mohamed Elneny ambae ametoka kwenye club ya Basel nchini Uswis na kujiunga na Arsenal. Hivi ni baadhi ya vitu kuhusu mchezaji huyu ambavyo ungependa kuvijua.

Amekulia kusini mwa Egypt na alionwa na scouts wa club ya Al Ahly na kumchukua kwenye academy. Ndani ya muda mfupi alikuwa mmoja kati wachezaji bora kwenye academy yao.

Alianza ku-shine akiwa na miaka 16 baada ya kujiunga na club ya El Mokawloon na kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza akiwa ndio mchezaji mdogo kuliko wote.

Anacheza defensive midfielder tangu akiwa El Mokawloon na kumudu vizuri hii nafasi, hii imekua moja ya factor zilizowavutia Arsenal na kumsajili.

Akiwa na miaka 20 alifanikiwa kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Basle na kucheza michezo karibia 100 na kusaidia club yake kushinda ubingwa wa ligi mara tatu mfululizo.

Hivi sasa ana miaka 23 na ana vigezo vya kucheza na Arsenal kwenye UEFA na anategemewa kuwa mchango mkubwa kwenye team.

Gharama yake kuwa ndogo (Pound milioni 5)na uwezo wake uwanjani pia vilimvutia kocha mchumi Arsenal Wenger kumleta mchezaji huyo ndani ya Emirates Stadium.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here