Home Kitaifa ALICHOKISEMA MAXIME BAADA YA KUSHINDWA KUTWAA MAPINDUZI CUP

ALICHOKISEMA MAXIME BAADA YA KUSHINDWA KUTWAA MAPINDUZI CUP

437
0
SHARE
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa pambano la fainali kati Mtibwa Sugar vs URA FC
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa pambano la fainali kati Mtibwa Sugar vs URA FC
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa pambano la fainali kati Mtibwa Sugar vs URA FC

Baada ya kupoteza mchezo wa fainali ya Mapinduzi Cup kocha mkuu wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime amesema amekubali matokeo ya mchezo huo kwa timu yake kulala kwa magoli 3-1 dhidi ya URA FC ya Uganda na kupoteza fainali ya pili mfululizo ndani ya miaka miwili.

Muda mfupi baada ya kumalizika kwa pambano la fainali Maxime amesema, amekubali kushindwa licha ya timu yake kucheza vizuri kwa kiwango cha juu.

“Mchezo wa mpira ndivyo ulivyo, unaweza ukacheza vizuri lakini usipate matokeo unayotarajia. Timu yangu imecheza vizuri lakini tumeshindwa kuibuka washindi wa mchezo wa fainali, mpira unamambo mengi, amesema nahodha huyo wa zamani wa Mtibwa na timu ya taifa ya Tanzania.”

Maxime ameongeza kuwa, mashindano ya mwaka huu yamekuwa ni mazuri licha ya kuwepo kwa kasoro chache ambazo kama zikifanyiwa kazi na kukirekebishwa itasaidia kuboresha mashindano hayo.

“Mashindano ya mwaka huu yamekuwa mazuri japo kulikuwa na mapungufu ya kawaida ambayo binadamu yeyote anaweza akafanya hata mimi pia pengine ningekosea lakini kama waandaji watayafanyia kazi mapungufu hayo basi huenda mashindano haya yakazidi kuwa bora siku zijazo.”

Fainali kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya URA ilikuwa ni ya tano kwa Mtibwa tangu mashindano hayo yaanze kutambulika rasmi mwaka 2007. Katika fainali zote ambazo Mtibwa imecheza, imefanikiwa kutwaa taji la Mapinduzi mara moja ambapo ilikuwa ni mwaka 2010 ilipoifunga timu ya Ocean View kwenye mchezo wa fainali uliopigwa kwenye uwanja wa Gombani, Zanzibar.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here