Home Ligi EPL TOP 5 YA WACHEZAJI WALIOKAMILISHA USAJILI WAO EPL

TOP 5 YA WACHEZAJI WALIOKAMILISHA USAJILI WAO EPL

1901
0
SHARE

done deal

Vikumbo vya usajili katika kipindi hiki cha dirisha dogo barani Ulaya vimeendelea wakati kila klabu ikitaka kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya kuhakikisha inapata matokeo mazuri kwenye michezo yake hasa katika kipindi cha lala salama cha raundi ya pili.

Hapa kuna list ya wachezaji watano ambao usajili wao tayari umekamilika na tayari wameshamwaga wino kuvitumikia vilabu vilivyowasajili.

5. Marko Grujic-Liverpool

Manager wa Liverpoo Jurgen Klop amekamilisha usajili wa star wa klabu ya Belgrade kujiunga na majogoo wa wekundu kwa dau la £5.1million kama ada ya uhamisho  wa mchezaji huyo.

Grujic

4. Jonjo Shelvey- Newcastle United

Shelvey-

Swansea City wamekubali kitita cha  £12m kama ada ya usajili wa wa nyota wao Jonjo Shelvey kujiunga na kikosi cha Newcastle United. nyota huyo wa kimataifa wa England sasa atajiunga na kocha  Steve Mc Laren katika dimba la St James Park

3. Henri Savet-Newcastle United

Saviet-Newca

Newcastle United imetangaza kumnasa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Bordeaux Henri Saivet kwa dau la £4.5m. Kiungo huyo ataungana na nyota wa kimataifa wa England  Shelvey katika dimba la St James Park.

2. Benik Afobe-Bounermouth

Klabu ya Bournemouth imetangaza kuinasa saini ya nyota wa zamani wa Arsenal Benik Afobe kwa kiasi cha £12million kutoka klabu ya Wolves ambayo kwa sasa inashiriki ligi daraja la kwanza (Championship) England.

Afobe

Nyota huyo raia wa England mwenye miaka 22 amefunga mabao 23 katika mechi 48 alizoicheea Wolves mwka 2015 zadi ya striker wa Tottenham Spurs Harry Kane.

Akiwa Emirates, aliweza kupachika kambani jumla ya magoli 20 kwenye mechi 13 aizoheza akiwa na timu ya U-18 lakini majeruhi yalirudisha nyuma maendeleo yake.

1. Steven Caulker-Liverpool

Steven-Caulker

Liverpool imekamilisha uhamisho wa beki wa Queens Park Rangers Steven Caulker kwa uhamisho wa mkopo wa miezi sita. nyota huyo wa kimataifa wa England alikuwa Sauthampton kwa mkopo lakini majeruhi ya mabeki wa Liverpool yamewasukuma kumsajili beki huyo kuziba nafasi za wachezaji walioumia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here