Home Kitaifa SIMBA YAMPA KERR MKONO WA KWAHERI, KOCHA MPYA AKABIDHIWA TIMU

SIMBA YAMPA KERR MKONO WA KWAHERI, KOCHA MPYA AKABIDHIWA TIMU

1216
0
SHARE

Kerr-Simba

Uongozi wa klabu ya Simba SC umevunja mkataba na aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi cha ‘wana Msimbazi’ Dylan Kerr pamoja na kocha wa makipaIddi Salim baada ya makubaliano ya pande zote mbili na kufikia uamuzi huo.

Makamu Mwenyekiti wa Simba SC Geofrey Ntyange ‘Kaburu’ amesema pande zote mbili (Simba SC na kocha Dylan Kerr) wamekubaliana kuvunja mkataba baada ya kukaa na kujadiliana kwa kirefu.

“Tumevunja mkataba na Kerr kwa makubaliano ya pande mbili baada ya kukaa na kujadiliana hatimaye tukafikia uamuzi huo”, amesema Kaburu ambaye alikuwepo Zanzibar akishuhudia mchezo kati ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar ambao Simba ilitupwa nje ya mashindano ya Mapinduzi katika hatua ya nusu fainali.

Makamu wa Rais wa klabu ya Simba Geofrey Nyange 'Kaburu' (katikati) akifatilia kwa karibu mchezo kati ya Simba dhidi ya Jamhuri kwenye moja ya mechi za Simba katika michuano ya Mapinduzi Cup
Makamu wa Rais wa klabu ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’ (katikati) akifatilia kwa karibu mchezo kati ya Simba dhidi ya Jamhuri kwenye moja ya mechi za Simba katika michuano ya Mapinduzi Cup

Katika hatua nyingine, kocha mpya wa klabu hiyo Jackson Mayanja ambaye amesaini mkataba na klabu hiyo siku chache zilizopita kama kocha msaidizi atachukua mikoba ya Kerr kwa muda wote ambao Simba itakuwa ikifanya mchakato wa kumpata mrithi wa Kerr.

Jackson Mayanja amekabidhiwa majukumu ya kukiongoza kikosi cha Simba katika kipindi ambacho mchakato wa kumpata kocha mkuu unaendelea
Kocha msaidi wa Simba Jackson Mayanja amekabidhiwa majukumu ya kukiongoza kikosi cha Simba katika kipindi ambacho mchakato wa kumpata kocha mkuu unaendelea

Leo asubuhi Dylan Kerr ali-tweet kwenye account yake ya twitter ujumbe ambao ulikuwa tafsiri nyingi kabla ya kuondoka visiwani Zanzibar kuelekea jijini Dar es Salaam ambapo inasemekana aliitwa kwa ajili ya kikao maalum na viongozi wa klabu ya Simba.

Huu hapa ni ujumbe ambao alipost kocha huyo muda mfupi kabla hajaiaha ardhi ya Zanzibar na kurejea jijini Dar.

IMG-20160112-WA0000

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here