Home Dauda TV KUTANA NA VIDEO NA PICHA ZA KING KIBA AKISIKITIKA BAADA YA YANGA...

KUTANA NA VIDEO NA PICHA ZA KING KIBA AKISIKITIKA BAADA YA YANGA KUTUPWA NJE YA MAPINDUZI CUP

3569
0
SHARE

Ally Kiba 6

Klabu ya Yanga imemsikitisha Star wa Bongo Flavor ‘King Kiba’ baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya timu ya URA ya Uganda.

Ally Kiba 3

Kiba alikuwepo jukwaani kuishuhudia mechi hiyo ya Yanga vs URA ambayo dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na ikabidi mshindi atafutwe kwa njia ya penati. Katika hatua ya changamoto za mikwaju ya penati Yanga ilijikuta ikiyaanga mashindano hayo kwa kutandikwa penati 4-3 na watoto wa Museveni.Ally Kiba 1

Goli la kusawazisha la URA lilimfanya Ally Kiba ashindwe kujizuia na kujikuta akitikisa kichwa kwa masikitiko mara baada ya Peter Lwasa kupachika mpira wavuni na kukatisha furaha ya wanajangwani ambao wengi wao walikuwa wakimcheka mnyama aliyenyolewa na Mtibwa kwenye mchezo wa mapema.

Ally Kiba 2

Ukiachana na kipaji cha kuimba, msanii huyo ambaye ameteka mashabiki lukuki wa Bongo, pia ni mchezaji mzuri wa soka na amekuwa anahudhuria mara kwa mara viwanjani kushuhudia mechi.

Dondoka hapa kucheki video fupi King Kiba akionekana kutoamini kilichoikuta Young Africans wakati ikichuana na URA kwenye mchezo wa nusu fainali ya Mapinduzi Cup.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here