Home Kitaifa CHEKI KOCHA MPYA WA SIMBA ALIVYOSHUHUDIA TIMU YAKE IKIKALISHWA NA MTIBWA-ZANZIBAR

CHEKI KOCHA MPYA WA SIMBA ALIVYOSHUHUDIA TIMU YAKE IKIKALISHWA NA MTIBWA-ZANZIBAR

1556
0
SHARE
Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja (kulia) akifatilia kwa makini mchezo wa nusu fainali kati ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar
Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja (kulia) akifatilia kwa makini mchezo wa nusu fainali kati ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar
Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja (kulia) akifatilia kwa makini mchezo wa nusu fainali kati ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Amaan, Zanziba.r Simba ililala kwa bao 1-0

Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja ameishuhudia timu yake mpya ikigaragazwa na Mtibwa Sugar na kuvurumishwa nje ya mashindano ya kombe la Mapinduzi kufuatia kuchezea kipigo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup inayoendelea visiwani Zanzibar.

Siku chache zilizopita uongozi wa Simba ulimtangaza Mayanja kuwa kocha mpya wa kikosi hicho kwa ajili ya kumsaidia Dylan Kerr kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Selemani Matola aliyekuwa kocha msadizi wa wekundu wa Msimbazi ambaye aliamua kujiuzulu kuendelea kuifundisha Simba kama kocha msaidizi.

Mayanja akiw makini akifatilia pambano la timu yake mpya ya Simba SC vs Mtibwa Sugar
Mayanja akiwa makini akifatilia pambano la timu yake mpya ya Simba SC vs Mtibwa Sugar

Mayanja alikuwa amekaa jukwaani huku akifatilia kwa makini mchezo wa Simba dhidi ya Mtibwa timu ambayo watakutana nayo kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara siku chache baada ya kumalizika kwa michuano ya Mapinduzi.

Mayanja 1

Mayanja amewahi kukinoa kikosi cha Kagera Sugar kwa mafanikio lakini kabla ya kutua Simba alikuwa akiifundisha timu ya Coastal Union ya jijini Tanga lakini tangu amejiunga na Costal Union hajakuwa na wakati mzuri kutokana na timu yake kuvurunda kwenye mechi za ligi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here