Home Kitaifa SIMBA, YANGA, NDANI YA BOTI MOJA KUREJEA DAR

SIMBA, YANGA, NDANI YA BOTI MOJA KUREJEA DAR

751
0
SHARE

Yanga -URA

Kilichomkuta Simba ndicho kimemkuta Yanga, watani hao wa jadi wamejikuta wakiambulia patupu kwenye michuano ya Mapinduzi Cup baada ya kuondoshwa kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Yanga wameshindwa kutamba baada ya kujikuta wakifuata nyayo za mnyama Simba kuyaaga mashindano ya Mapinduzi kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya URA ya Uganda kufuatia timu hizo kutoka sare ya kufungana goli 1-1 kwenye dakika 90 za mchezo huo uliopigwa usiku wa Jumapili January 10, 2016.

Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Amis Tambwe dakika ya 13 kipindi cha kwanza ambaye aliunganisha kwa kichwa mpira uliotemwa na golikipa wa URA wakati akitaka kuokoa mpira wa kichwa uliopigwa na Simon Msuva.

Yanga-URA 1

Lakini URA walikuja juu na kusawazisha goli hilo dakika ya 76 mfungaji akiwa Peter Lwasa aliyeipa timu yake matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Dakika 90 zikamalizika kwa sare ya bao 1-1, kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, baada ya dakika 90 kumalizika huku kukiwa hakuna mshindi zinapigwa penati kutafuta mshindi wa mchezo.

Katika changamoto za mikwaju ya penati Yanga walifanikiwa kufunga penati 3 huku wachezaji wao wakipoteza mikwaju miwili ya penati wakati URA wao walikwamisha kambani penati 4 na kupoteza penati moja.

Yanga-URA 2

Mpira ulikuwa ni wa kasi mwanzo-mwisho kutokana na timu zote kushambuliana kwa kupokezana, lakini Yanga walijikuta wakikimbizwa katika dakika 20 za mwisho hali iliyopelekea kukubali kuruhusu waganda kupata goli la kusawazisha.

Kutolewa kwa Yanga na Simba kwenye hatua ya nusu fainali kunazifanya ziungane na Azam FC ambayo iliaga mashindano kwenye hatua ya makundi na kufanya ziwe timu tatu za ligi kuu Tanzania bara zilizoshindwa kutamba kwenye michuano hiyo.

Mtibwa ndiyo itaiwakilisha Tanzania kwenye fainali ya Mapinzuzi Cup siku ya Jumatano January 13, 2016 siku moja baada ya kilele cha maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Yanga-URA 3

Waliopata penati za Yanga: Kelvin Yondani, Simon Msuva na Deogratias  Munish

Walipoteza penati upande wa Yanga: Geofrey Mwashiuya na Malimi Busungu

Walifunga penati za URA: Jimmy Kulaba, Said Kyeyune, Deo Otieno na Bwete Brian

Aliyekosa penati ya URA: Sekito Sam

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here