Home Kitaifa MKWASA: “SAMATTA AENDE ULAYA KUFANYA ALIYOYAFANYA AFRIKA”

MKWASA: “SAMATTA AENDE ULAYA KUFANYA ALIYOYAFANYA AFRIKA”

539
0
SHARE

Charles Mkwasa

 Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa amesema, tuzo naliyoshinda mchezaji wake ni somo kwa wachezaji wengine vijana ambao wanandoto za kufikia mafanikio yaliyofikiwa na Samatta hadi sasa kwenye mchezo wa soka.

Wakati huohuo Mkwasa amemtaka Samatta kwenda kudhihirisha ubora wake Ulaya kwa kufanya yote ambayo ameyafanya Afrika ikiwa ni pamoja na kupachika mabao kambani. Kocha hu amesema sasa atafute mbinu za kuwania tuzo ya mchezaji bora Afrika kwasababu tayari ameshaonesha uwezo ndani ya Afrika hivyo apambane na akina Toure na Aubameyang kuwania tuzo ya Afrika kwa ujumla.

Mtandao huu umekutana na Mkwasa isiwani Zanzibar kwenye michuano ya Mapinduzi Cup inayoendelea visiwani hapa huku Mkwasa akiwa anafatilia michuano hiyo kwa jicho la karibu ili kuweza kubaini vipaji vipya pamoja na viwango vya wacheaji wengine kwa ajili ya kujenga na kuboresha kikosi cha Stars ambacho siku siku chache zijazo kitacheza mechi za kuwania kufuzu kucheza michuano ya kombe la dunia pamoja na michuano ya Mataifa ya Afrika.

Mkwasa ameongeza kuwa, alikuwa anamuombea Samatta kilasiku ili ashinde tuzo hiyo lakini alikuwa na hofu huenda kungekuwa na upendeleo kwa kanda ya Afrika ya Kaskazini.

Mazungumzo kati ya shaffihdauda.co.tz na Charles Boniface Mkwasa yalikuwa hivi…

Shaffihdauda.co.tz: Ukiwa kama kocha unayemfundisha Mbwana Samatta kwenye timu ya taifa, umepokeaje taarifa za mchezaji wako kutwaa tuzo ya Afrika kwa wachezaji wa ndani?

Mkwasa: Nianze kwa kusema ni faraja kwake na faraja kwetu sisi watanzania, ni heshima kwa  nchi kwasababu ameitangaza vizuri nchi yetu katika soka pengine watu wengi hawaijui Tanzania kama kunavipaji vya mpira kwahiyo hiyo inainua kiwango na inatangaza nchi, ni faraja kubwa kwetu.

Shaffihdauda.co.tz: Wakati unapiga kura yako, ulitarajia kama Samatta atashinda na kutwaa tuzo hiyo?

Mkwasa: Mimi kilasiku nilikuwa namuombea kwasababu tittle ambayo amepata yeye ni kutokana na mashindano ya vilabu bingwa vya Afrika mpaka unakuwa mfungaji bora ni kazi kubwa umeifanya kwahiyo mimi nilikuwa natarajia kwamba ataipata isipokuwa nilikuwa nawasiwasi na ule uafrika wa kikanda huenda wangefanya upendeleo lakini kwa ujumla mimi nilikuwa namuombea apate na amepata namshukuru Mungu.

Shaffihdauda.co.tz: Wachezaji wengine wa kitanzania wajifunze nini kupitia kwake?

Mkwasa: Nafikiri ni lesson kwa vijana wengine ambao wanacheza na wanahitaji kuiga mfano wake na wajifunze kutoka kwake lakini siwezi kuwasemea wao lakini naamini watakuwa wamejifunza na itawapa mwangaza mzuri wengine wenye nia ya kutaka kuendelea.

Shaffihdauda.co.tz: Ukiwa kama kocha unamuona wapi Samatta baada ya miaka mitatu ijayo na unamshauri nini?

Mkwasa: Sasahivi angaalie mbele kwasababu anakwenda kucheza Ulaya, pengine timu atakayokuwa anakwenda kucheza inaweza kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Confederation au UEFA Champions League kwahiyo afanye kazi na akipata nafasi nzuri ashindane na akina Toure na Aubameyang kwasababu kwa Afrika huku amesha prove anaweza kwahiyo atakapokwenda Ulaya ajitahidi kufanya haya aliyoyafanya Afrika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here