Home Kitaifa EXCLUSIVE: KUTANA NA ABDI KASSIM ‘BABI’ MWENYE REKODI AMBAYO HAITAVUNJWA NA MCHEZAJI...

EXCLUSIVE: KUTANA NA ABDI KASSIM ‘BABI’ MWENYE REKODI AMBAYO HAITAVUNJWA NA MCHEZAJI YEYOTE DUNIANI

1463
0
SHARE
Abdi Kassim 'Babi' kwa sasa yupo visiwani Zanzibar baada ya mkataba wake na klabu aliyokuwa anaitumikia nchini Malaysia kumalizika
Abdi Kassim 'Babi' kwa sasa yupo visiwani Zanzibar baada ya mkataba wake na klabu aliyokuwa anaitumikia nchini Malaysia  kumalizika
Abdi Kassim ‘Babi’ kwa sasa yupo visiwani Zanzibar baada ya mkataba wake na klabu aliyokuwa anaitumikia nchini Malaysia kumalizika

Asikwambie mtu hakuna kitu kizuri kama kuandika historia ambayo haitafutika kwenye maisha hasa pale historia hiyo inapokuwa nzuri na inagusa maisha ya watu wengi moja kwa moja na kuwafanya wakukumbuke vizazi hadi vizazi.

Nikiwa hapa visiwani Zanzibar kufatilia michuano ya Mapinduzi Cup, mara nakutana na mkongwe wa soka la Tanzania Abdi Kassim ‘Babi’ Ballack wa Unguja na kuamua kufanya nae mahojiano maalumu kutokana na umuhimu wake katika soka la Bongo.

Huyu jamaa ndiye alifunga bao la kwanza kabisa kwenye uwanja mpya wa taifa na kuandika historia isiyofutika katika medani ya soka nchini Tanzania.

Haya ndiyo yalikuwa majibu ya Babi alipokuta uso kwa uso na maswali ya shaffihdauda.co.tz

Shaffihdauda.co.tz: Unajisikiaje kuwa mchezaji uliyefunga goli la kwanza kwenye uwanja mpya wa taifa jijini Dar es Salam na goli hilo lina maana gani kwako?

Babi: Hiyo ni faraja kubwa kwangu kwasababu kila napohojiwa na waandishi wa habari mara nyingi huwa wananiuliza jambo hilo. Hiyo ni historia ambayo ipo na itazidi kuwepo hata kama mimi sitakuwepo tena lakini historia itabaki hata vizazi vizavyo vitaikuta historia iko hivyo kwahiyo mimi najivunia hilo na siwezi kusahau najisikia furaha hadi leo.

Kufunga goli lile ilikuwa ni jambo jema sana kwangu kwasababu watanzania walikuwa wamejaa uwanjani. Ni goli ambalo liliniongezea kujulikana na kujenga jina lakini kitu ambacho kinanipa faraja ni kubaki kwenye historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao la kwanza kwenye uwanja ule.

Shaffihdauda.co.tz: Kwasasa maisha yako ya soka yakoje maana ligi nyingi bado zinaendelea lakini wewe upo nyumbani unakula bata Zanzibar

Babi: Mimi bado naenelea na soka lakini mkataba wangu na timu ya Malaysia umemalizika kwahiyo sasahivi nipo likizo lakini kwa sasa nipo kwenye maandalizi ya kujiweka fiti muda wote naweza nikahitajika na timu yoyote kwasababu tayari kuna offer nyingi ziko mezani.

Kwa muda huu ambao niko Zanzibar nimejiunga na timu ya KMKM ya hapa Zanzibar kwa muda mfupi mpaka hapo nitakapopata timu nyingine.

Shaffihdauda.co.tz: Hadi sasa ni timu gani ambazo zimeonesha nia ya kukutaka na tayari zimeweka offer mezani?

Babi: Kwa nje ya Tanzania zipo nyingi tu ambazo nyingine sizifahamu kwasababu nina manager ambaye yupo Malaysia, tunawasiliana na ananimbia kuna timu za Malaysia, Indonesia na Thailand ambazo zimeniona na wanahitaji nikacheze kwao.

Kwa hapa Tanzania kuna timu zipo lakini zinaogopa kwasababu wanajua huyu mtu safari yake ipo mbele lkini zipo, labda zinasubiri mpaka nitakaposema sasahivi sihitaji tena kucheza professional nataka kucheza nyumbani ndiyo watakuwa tayari kunifata.

Lakini mimi siangalii kucheza professional tu, naangalia sehemu yeyote yenye maslahi hata kama kuna timu nitakayoona ina maslahi Zanzibar au bara mimi nasajili.

Babi alivyoweka rekodi ambazo hazitafutika kwenye soka la Tanzania

Babi aliandika historia ya kufunga bao la kwanza kwenye uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ uliochezwa September 1, 2007 na kuipa Stars ushindi wa bao 1-0. Mchezo huo ulikuwa ni maalum kwa ajili ya ufunguzi wa uwanja huo ambao umejengwa kwa mabilioni ya shilingi.

Rekodi hiyo haiwezi kuvunjwa na mchezaji yeyote duniani labda uwaja wa taifa uvunjwe na kujengwa uwanja wingine mpya.

Hata hivyo, Babi aliweka rekodi nyingine baada ya kuifungia Azam bao la kwanza katika mchezo wa kimataifa wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Nasri ya Sudan Kusini, wakati Azam ilipopata ushindi wa magoli 3-1, mechi hiyo ilichezwa February 2013 kwenye Uwanja wa taifa, Dar es Salaam.

Babi ndiye aliyefungua ukurasa mpya kwa timu hiyo kuiwezesha kupata ushindi katika mechi za kimataifa, wakati Azam FC ikishiriki kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.

Endelea kufatilia mtandao huu kwani utakuletea sehemu ya pili ya mahojiano na mchezaji huyo ili kukupa vitu vingi zaidi ambavyo huenda huvifahamu kuhusiana na maisha yake ya soka.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here