Home Ligi EPL ARSENAL WANAAMINI STRIKER HUYU WA AFRIKA ATAWASAIDIA KUTWAA NDOO YA EPL MSIMU...

ARSENAL WANAAMINI STRIKER HUYU WA AFRIKA ATAWASAIDIA KUTWAA NDOO YA EPL MSIMU HUU

645
0
SHARE

Odion Ighalo

Klabu ya Arsenal inawania saini ya mshambuliaji raia wa Nigeria Odion Ighalo anayekipiga Watford inayoshiriki ligi kuu soka nchini England, katika harakati za kukiongezea nguvu kikosi chao msimu huu ili kuhakikisha wanapata chochote mwisho wa msimu.

Maskauti wa Arsenal chini ya kocha Arsene Wenger wanatafuta mshambuliaji atakayeongeza magoli katika safu yao ya ushambuliaji na kuona kuwa Odion Ighalo zao la Academy ya Manchester United anaweza kufiti katika mahitaji yao.

Odion Ighalo ameshafunga mabao 14 katika mechi 20 ambazo amecheza hadi sasa kwenye raundi ya kwanza ya ligi kuu England
Odion Ighalo ameshafunga mabao 14 katika mechi 20 ambazo amecheza hadi sasa ikiwa ni msimu wake wa kwanza kwenye ligi kuu ya England

Tayari mambo anayoyafanya mshambuliaji huyo kutoka Nigeria yamekua katika rekodi za watu kwani tayari Odion Ighalo ameifungia klabu yake ya Watford magoli 14 katika msimu huu na kuongeza thamani yake katika dirisha hili la usajili.

Lakini Ighalo mwenyewe amekaririwa akisema kuwa itakua ngumu kwake kukataa ofa ya kuichezea klabu aliyokulia ya Manchester United endapo tu kocha Louis Van Gaal atataka huduma ya mshambuliaji huyo ambaye anawataja Dwight Yorke na Andy Cole kama mashujaa wake akiwa Old Trafford.

Aubamechicha

Wakati huo huo klabu ya Arsenal inaangalia uwezekano wa kumnasa mshambuliaji Pierre-Emmerick Aubamayang wa Borussia Dortmund ama mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, mmexico Javier Hernandez ‘Chicharito’.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here