Home Kitaifa BAADA YA TAARIFA ZA USHINDI WA SAMATTA KUMFIKIA RAIS MAGUFULI

BAADA YA TAARIFA ZA USHINDI WA SAMATTA KUMFIKIA RAIS MAGUFULI

483
0
SHARE

Screen Shot 2016-01-08 at 1.25.24 PM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ameungana na watanzania wote kusherekea na kutuma salamu za pongezi kwa Mbwana Samatta ikiwa ni siku moja tu baada ya nyota huyo kutangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Rais Magufuli ametuma salamu za pongezi kwa Samatta kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Mh. Nape Nnauye. Taarifa hiyo iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa, Magufuli amesema Samatta amejijengea heshima pamoja na kuiletea heshima Tanzania.

Jana usiku January 7, 2015 Samata alishinda tuzo hiyo Abuja, Nigeria na kuwa mtanzania wa kwanza kushinda tuzo hiyo yenye heshima kubwa Afrika na nje ya Afrika.

Taarifa ya Ikulu kwenda kwa Waziri Nape Nnauye inasomeka hivi….

Magufuli-pongezi

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here