Home Kitaifa EXCLUSIVE: PAUL NONGA AFICHUA SIRI ILIYOFICHIKA NYUMA YA JEZI NAMBA 26 NI...

EXCLUSIVE: PAUL NONGA AFICHUA SIRI ILIYOFICHIKA NYUMA YA JEZI NAMBA 26 NI BAADA YA MKEWE KUJIFUNGUA MTOTO DECEMBER 26, JINA LA MTOTO NA MAMBO MENGINE PIA HADHARANI

724
0
SHARE
Nonga Junior akiwa amepumzika
Nonga Junior akiwa amepumzika
Nonga Junior akiwa amepumzika

Mchezaji mpya wa Yanga ameingia kwenye rekodi kadhaa tangu kujiunga na klabu hiyo ya Jangwani. Nonga ambaye anavaa jezi namba 26 mgongoni, mkewe alijifungua mtoto wa kiume December 26, 2015 siku ya Boxing Day lakini tarehe hiyo ni sawa na namba ya jezi ambayo inavaliwa na baba wa mtoto huyo.

Siku hiyo Nonga alikuwa anacheza mechi yake ya kwanza ya mashindano tangu ajiunge na Yanga akitokea Mwadui FC ya Shinyanga.

Mtandao huu umepiga story na Nonga ambaye yupo Zanzibar kwenye mashindano ya kombe la Mapinduzi kutaka kujua nini kipo nyuma ya namba 26 pamoja na mambo mengine yanayohusu maisha ya soka ya nyota huyo wa zamani wa Mbeya City FC.

Mama Nonga Jr akimbembeleza mwanaye
Mama Nonga Jr akimbembeleza mwanaye

Shaffihdauda .co.tz: Umefanikiwa kufunga goli kwenye mchezo wa kwanza wa Yanga wa michuano ya Mapinduzi Cup lakini likiwa ni goli lako la kwanza kwa Yanga kwenye mechi ya mashindano, unajisikiaje kwa hilo?

Paul Nonga: Namshukuru Mungu kwa dakika ambazo nilipewa na maelekezo ambayo mwalimu alinipatia wakati naingia, niliweza kufanya kama vile ambavyo yeye alitaka kwayiho ilikuwa ni furaha kwa Yanga na wapenda soka wote. Pia nashukuru kuwepo hapa kwasababu Yanga wamenipokea vizuri na hicho kitu kimenifanya nisichukue muda mrefu kwenda na kasi ya yao.

Kwa Yanga ilikuwa ni mechi yangu ya tatu, mechi yangu ya kwanza ilikuwa dhidi ya Friends Rangers nikafunga magoli mawili, mechi yangu ya pili tulicheza na Mbeya City (ligi kuu) sikuweza kufunga na mechi ya tatu ni ndiyo ya Mapinduzi Cup dhidi ya Mafunzo.

Shaffihdauda .co.tz: Wewe kwa upande wako unazungumziaje uhamisho wako kutoka Mwadui FC kwenda Yanga?

Paul Nonga: Siku zote unapokuwa unafanya kitu lazima uwe na plan, mpira wa Tanzania mara nyingi sana unakuwa umetawaliwa na hizi timu kongwe mfano mzuri ni sasahivi, Simba, Yanga na Azam wapo hapa Zanzibar wanacheza Mapinduzi lakini kuna baadhi ya timu zipo mapumzikoni hii ni faida kubwa kwa mchezaji kwasababu anapata nafasi ya kucheza mechi nyingi na mashindano mengi.

Bado kuna mashindano ya kimataifa ambayo nayaweza kumfanya mchezaji kuonekana nje ya mipaka ya Tanzania.

Jacky Nonga akimpumzisha Nonga Junior
Jacky Nonga akimpumzisha Nonga Junior

Shaffihdauda .co.tz: Tukiachana na hayo mengine, wewe unavaa jezi namba 26 mgongoni jezi hii imebeba siri gani?

Paul Nonga: Hii namba nilitokea tu kuipenda lakini ni upande wa pili wa namba 13 ambayo naipenda pia ukiachana na namba 17 ambayo ndiyo tarehe ya kuzaliwa kwangu. Kwahiyo ninanamba tatu ambazo huwa zipo kwenye kichwa changu, sehemu yeyote nikienda nikikosa namba 13 nitachukua namba 26 na nikikosa namba 26 basi nitalazimika kuvaa jezi namba 17 ambayo ni tarehe yangu ya kuzaliwa.

Shaffihdauda.co.tz:  Decemer 26 mkeo alijifungua mtoto wa kiume. Kuna uhusiano gani kati ya namba yako ya jezi na tarehe ya kuzaliwa kwa mtoto wako?

Paul Nonga: Ni kweli nilipata mtoto wife alijifungua siku ambayo mimi nacheza mechi yangu ya kwanza ya mashindano nikiwa Yanga ambayo tulicheza na Mbeya City. Ilikuwa ni tarehe 26. 12. 2015 mimi mwenyewe navaa jezi namba 26, kuna kitu ambacho mtu anaweza kukifikiria kwasababu mtoto amezaliwa siku ya Boxing Day ni moja ya vitu ambavyo havitafutika kwenye akili yangu.

Mama Nonga Jr enzi zake wakati akiwa mama kijacho
Mama Nonga Jr enzi zake wakati akiwa mama kijacho

Shaffihdauda .co.tz: Mwanao umempa jiana gani?

Paul Nonga: Mwanagu anaitwa Nonga Junior

Shaffihdauda .co.tz: Kwa nini umeamua kumuita jina hilo na lina maana gani kwake?

Paul Nonga: Hilo jina mimi na wife tulipanga kumpa hata kabla hajazaliwa. Nadhani anaweza akawa Nonga mwingine anayekuja, namuona kabisa anakuja kuwa footballer.

Paul Nonga akiwa na mkewake Jacky Paul Nonga akimfariji wakati wa ujauzito wake
Paul Nonga akiwa na mkewake Jacky Paul Nonga akimfariji wakati wa ujauzito wake

Shaffihdauda .co.tz: Umebadilisha mazingira kutoka Mwadui FC kwenda Yanga SC, hii inaweza kuwa changamoto kwako, umejipangaje kuhakikisha unapata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza ambacho kiawachezaji wengi wazuri wa nafasi unayocheza wewe?

Paul Nonga: Kweli changamoto ni kubwa lakini mimi huwa napenda sana kushindana na siogopi kushindana, wakati naenda Yanga nilikuwa najua kabisa Yanga ni timu nzuri na timu kubwa na kongwe inayotaka mafanikio na yenye wachezaji wazuri kuliko hata mimi na hilo mimi nakiri hasa kwa nafasi yangu.

Kwahiyo siku zote unapotaka kufanikiwa kwenye kitu chochote, hutakiwi kuogopa kujifunza. Mimi nililitambua hilo na kwangu ni changamoto sana na inanifanya nifanye kazi kwa bidii ili niweze kuwa mmoja kati ya watoa msaada katika timu ya Yanga.

Screen Shot 2016-01-02 at 11.22.08 AM

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here