Home Dauda TV MGOMO BARIDI WAMSAIDIA SAMATTA KUPATA GARI SIMBA

MGOMO BARIDI WAMSAIDIA SAMATTA KUPATA GARI SIMBA

623
0
SHARE

Mbwana Samatta 1

Moja ya kero kubwa za jiji la Dar es Salaam ni usafiri, hasa usafiri wa daladala ambao unatumiwa na watu wengi ambao hawana uwezo wa kununua magari yao binafsi ili kuweza kuwafikisha kwenye maeneo wanayohitaji kufika.

Mbwana Samatta wakati anaanza soka alikuwa analazimika kutumia usafiri wa daladala kutoka nyumbani kwenda uwanjani kwa ajili ya mazoezi na kurudi. Kero zitokanazo na usafiri huu zilimfanya Samatta atamani kuwa na gari lake binafsi kwa ajili ya kumwezesha kufanya safari zake kwa uhuru zaidi na kwa muda sahihi.

Njia pekee ya yeye kupata gari ilikuwa ni wakati anasajiliwa kutoka African Lyon kwenda Simba. Samatta anasema moja ya masharti yake lilikuwa ni kupatiwa gari kwa ajili ya kutembelea na hilo lilikubaliwa na uongozi wa Simba. Lakini kimbembe ilikuwa ni kulipata gari hilo baada ya kusaini mkataba, hapa zikaanza danadana hadi akaamua kutia mgomo baridi hadi hapo atakapopatiwa usafiri wake.

Walinipa contract ilikuwa ya pesa, lakini kipindi hicho nilikuwa natamai siku moja kuwa na gari niachane na pilikapilika za daladala. Nikawaambia kwenye hii contract waweke kipengele cha kuninunulia gari, wakakubali na kusema hilo halina tatizo gari nitapata pamoja na kiasi cha pesa, tukakubaliana mimi nikasaini.

Lakini tukawa tumewekeana muda baada ya muda flani natakiwa niwe nimeshapatiwa gari, lakini ule muda ukapita nikiwa bado sijapatiwa gari na wakati huo nikiwa tayari nimeshasaini mkataba. Viongozi wengine wote wakawa hawana habari tena na mimi isipokuwa kiongozi mmoja tu ndiye alikuwa ananifatilia kwa karibu zadi kwasababu ndiye aliyewasilisha suala la mimi kusajiliwa na Simba.

Suala la mimi kukataa kuijunga na timu lilikuwa kwenye gari tayari tulikuwa tumeshasaini mkataba lakini nilikuwa siwezi kujiunga mpaka vitu vyote vilivyopo kwenye mkataba viwe vimekamilika kwasababu nilikuwa nasikia wachezaji wengi wanaocheza kwenye vilabu hivyo hawatimiziwi haja zao kama wanavyokuwa wameandika kwenye mikataba.

Kwahiyo ili suala hilo lisijirudie kwangu mimi kwasababu tayari nilikuwa naona mifano nikawaambia wamalize kila kitu kilichoandikwa kwenye mkataba baada ya hapo mimi sitokuwa na shina na wao. Labda kwasababu walikuwa wananichukulia mchezaji mdogo ambaye nilikuwa natamani siku moja kucheza kwenye vilabu hivi. Kwasababu tukiwa wadogo tunatamani kucheza kwenye vilabu ambavyo kilasiku tutakuwa tunatajwa na kusika.

Wakati huo tunaamini huko ndiko kwenye maslahi mazuri tunaweza kujenga maisha, basi mimi nilichoamua ni kukaa nyumbani kwasababu walikuwa hawataki kutima masuala ya kwenye makataba. Kwa kipindi hicho nilikuwa bado mdogo sana na nilikuwa nimesaini mkataba wa miaka miwili. Kwasababu ya udogo wangu, muda mwingine nikawa nafikiria naweza kukaa nje miaka miwili na nikaja kucheza tena soka.

Bado nikawa naendelea kuwasisitiza viongozi wa Simba wanipe hiyo gari bila kujali wamelinunua kwa thamani ya kiasi gani ila nataka gari ili niweze kutumia. Walileta usumbufu kidogo, karibu duru la kwanza la ligi likaisha nikiwa bado sijapatiwa gari.

Bada ya duru la kwanza kumalizika wakakaa wakakubaliana wanipe gari, wakanifata wakaniambia duru la kwanza limeisha tunataka duru la pili utumikeutapewa gari. Nikasainiana mkataba na mtu ili nianze mazoezi lakini ikitokea hadi siku flani nikiwa sijapata gari basi niupeleke mkata hata kwenye vyombo vya habari.

Nikaanza mazoezi na timu nikacheza na mechi ya kirafiki mechi yangu ya kwanza nikiwa na simba ilikuwa na FC Leopard, tulishinda kwa magoli mawili mimi nilifunga goli la kwanza na Mohamed Shiboli alifunga goli moja. Baada ya hapo tukasafiri kwenda kwenye mapinduzi Zanzibar lakini kwasababu mwalimu tayari alikuwa na timu yake, ilikuwa ngumu sana kunitumia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here