Home Kimataifa LEBRON AWEKA REKODI, IRVING AIONGOZA CAVALIERS KUICHAPA PHOENIX SUNS..

LEBRON AWEKA REKODI, IRVING AIONGOZA CAVALIERS KUICHAPA PHOENIX SUNS..

410
0
SHARE

lebron

Inawezekana kabisa mchezaji Lebron James taratibu akawa anaachia kijiti kwa wachezaji wengine kama Kevin Durant, Stephen Curry , James Harden na kina Anthony Davis. Lakini kuna upande ambao bado anautendea haki upande wa pili ambao ni kuweka rekodi.

Alfajiri ya leo, Lebron James aliweka rekodi ya kupanda mpaka katika nafasi ya 17 kwenye orodha ya ufungaji bora wa muda wote. Lebron alimshusha Alex English katika orodha hiyo. Lakini pia hakuishia hapo, Lebron pia alimshusha mchezaji Stephon Marbury katika nafasi ya 22 ya wachezaji waliokuwa na pasi/assists nyingi zaidi.

Katika huu uliomalizika kwa ushindi wa 101-97, mchezaji Kyrie Irving alionekana kuanza kurejea taratibu katika ubora wake. Kyrie Irving aliiongoza Cavaliers kwa kufunga pointi 22, J.R Smith akaongeza pointi 17 huku Kevin Love akifunga pointi 16.

T.J Warren yeye aliiongoza Phoenix Suns kwa kufunga pointi 23 huku Brandon Knight akiongeza nyingine 18.

HIGHLIGHTS

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here