Home Kimataifa REKODI MBALIMBALI ZILIZOWEKWA MPAKA SASA KATIKA NBA MSIMU 2015/16.. PART TWO

REKODI MBALIMBALI ZILIZOWEKWA MPAKA SASA KATIKA NBA MSIMU 2015/16.. PART TWO

641
0
SHARE

CUR

Novemba 23, 2015, LeBron James aliingia katika orodha ya wachezaji 25 wa muda wote waliotoa pasi/assists nyingi. Hi ilimfanya kujiunga na Oscar Robertson kama wachezaji pekee katika historia ya NBA kuwa katika top-25 katika wingi wa pointi na pasi/assists.

Novemba 24, 2015, Golden State Warriors iliweka rekodi katika NBA kuwa timu iliyoshindamichezo mingi zaidi tangu kuanza kwa ligi 16-0 kufuatia ushindi dhidi ya Los Angeles Lakers. Warriors hatimaye walianza  msimu na rekodi ya 24-1 baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Milwaukee Bucks Desemba 12, 2015. Mpaka sasa wana rekodi ya 28-1.

KOBE

Novemba 29, 2015, Kobe Bryant alitangaza angeweza kustaafu mwisho wa msimu. Katika kipindi hiki cha msimimu ishirini, Bryant alishinda mataji 5 ya NBA, tuzo moja ya MVP, na alichaguliwa kushiriki All-Star Game mara kumi na saba.

Philadelphia 76ers ikawa timu ya kwanza katika historia ya ligi kuanza misimu miwili mfululizo na rekodi ya 0-17.  Pia ikaishia kuvunja rekodi ya NBA kupoteza michezo mingi zaidi mfululizo, 28 wakiungana na  New Jersey Nets katika msimu wa 2009-10 kabla ya kupata ushindi wao wa kwanza msimu huu Desemba 1 2015 nyumbani dhidi ya Los Angeles Lakers.

Novemba 30, 2015, Dirk Nowitzki alipata mtupo wake wa 10000 katika mchezo waliopoteza dhidi ya Sacramento Kings. Amekuwa mchezaji wa 13 katika historia ya NBA kufikia hatua hiyo.

Desemba 1, 2015, Kevin Garnett alimfikia mchezaji wa zamani na kocha wa sasa wa  Milwaukee Bucks Jason Kidd katika nafasi ya  tatu kwa wachezaji waliocheza zaidi  katika historia ya ligi kwa kucheza kwa dakika 20 katika mchezo dhidi ya  Orlando Magic.

Garnett akiwa na Kidd wakati akichezea Brooklyn Nets huku Kidd akiwa kocha wake
Garnett akiwa na Kidd wakati akichezea Brooklyn Nets huku Kidd akiwa kocha wake

 

Boston Celtics ikacheza dhidi ya Sacramento Kings Desemba 3, 2015 kule nchini Mexico katika uwanja wa Mexico City Arena, na Celtics kushinda 114-97.

Desemba 5, 2015, Kevin Garnett aliweza kufikia jumla ya pointi  26000  katika mchezo ambao Timberwolves ilipoteza kwa Trail Blazers.

Desemba 5, 2015, Rajon Rondo akaweza kutoa pasi yake ya  5000 katika historia yake ya NBA ingawa timu yake ilipoteza dhidi ya Rockets.

Desemba 5, 2015, Pau Gasol alicheza katika mechi yake ya 1000 kwenye mchezo waliopoteza dhidi ya  Hornets.

Desemba 9, 2015, Chris Paul alitoa pasi 18 katika ushindi dhidi ya Bucks, hii ilimfanya kumpita Tim Hardaway, Sr. katika nafasi ya 14 katika orodha ya wachezaji waliotoa assits nyingi zaidi.

paul

Desemba 11, 2015, Kevin Garnett akawa mchezaji aliyedaka  rebounds nyingi zaidi za ulinzi (defensive rebounds) katika historia ya NBA.Alimpita mchezaji wa zamani Karl Malone.

Desemba 16, 2015, Paul Pierce alifunga pointi nakuweza kufikia idadi ya pointi  26000 katika mchezo dhidi ya Bucks.

Desemba 21, 2015, Chris Paul alitoa  pasi 10 wakifungwa  100-99 nyumbani kwa Oklahoma City Thunder. Hii ilimfanya ampite Terry Porter katika nafasi ya 13 orodha ya muda wote ya wachezaji waliotoa assists nyingi.

Desemba 23, 2015, Dirk Nowitzki alimpita Shaquille O’Neal katika nafasi ya 6 katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa NBA. Alifunga pointi 22 wakati klabu yake ya Dallas Mavericks ‘ ikishinda 119-118 katika muda wa nyongeza dhidi ya Brooklyn Nets.

dirk

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here