Home Dauda TV BAADA YA KUPIGWA 4 ARSENAL YAJIPOZA, MAN U, CHELSEA, ZASHINDWA KUTAMBA

BAADA YA KUPIGWA 4 ARSENAL YAJIPOZA, MAN U, CHELSEA, ZASHINDWA KUTAMBA

642
0
SHARE

Man U vs Chelsea

December 29, 2015 imepigwa michezo nane ya ligi kuu ya England ikiwa ni michezo ya raundi ya 19 ambayo ni nusu ya michezo yote ya msimu wa 2015-2016.

Katika michezo yote iliyopigwa leo, michezo miwili ilikuwa inatazamwa kwa jicho la karibu na wapenzi wengi na mashabiki wa soka. Michezo hiyo ni kati ya Arsenal vs Bournemouth na Manchester United vs Chelsea.

Mchezo kati ya Arsenal dhidi ya Bournemouth umemalizika kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa maoli 2-0 wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Emirates. Ushindi huo ni faraja kubwa kwa The Gunners kwani mchezo wao wa weekend iliyopita walijikuta wakiloa kwa bao 4-0 mbele ya Southampton

Magoli ya Arsena yamekwamishwa kambani na Gabriel Paulista aliyefunga goli la kwanza dakika ya 27 wakati Mesut Ozil alifunga bao la pili na kuihakikishia Arsenal ushindi wakiwa kwenye dimba lao la nyumbani.

Manchester United na Chelsea zimeshindwa kutambiana baada ya timu hizo kutoka sare ya bila kufungana licha ya kila timu kutafuta ushindi katika mchezo wa leo, lakini magolikipa wa timu zote mbili walifanya kazi za ziada kuzisaisia timu zao zisiruhusu magoli kwenye mchezo huo.

Matokeo ya leo yanaifanya Arsenal kuongoza ligi kwa muda ikisubiri matokeo ya mchezo kati ya Manchester City dhidi ya Leicester Ciyt. Endapo Leicester City watashinda mchezo huo wataendelea kukaa kileleni mwa ligi kwasababu watakuwa wamefikisha jumla ya pointi 41 wakiiacha Arsenal kwa pointi mbili. Lakini ikiwa mchezo huo utamalizika kwa sare Arsenal itakaa kileleni kwa tofauti ya pointi na ikitokea imepoteza mchezo huo itabaki nafasi ya pili kwenye msimamo.

Maokeo ya michezo yote iliyopigwa December 28 ni kama ifuatavyo:

Crystal Palace 0-0 Swansea

Everton 3-4 Stoke

Norwich 2-0 Aston Villa

Watford 1-2 Tottenham

West Brom 1-0 Newcastle

Arsenal 2-0 Bournemouth

Man Utd 0-0 Chelsea

West Ham 2-1 Southampton

Video ya magoli yote ya Arsenal vs Bounermouth

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here