Home Dauda TV DAUDA TV: HIVI NDIVYO ARSENAL ILIVYOSHINDWA KUKWEA KILELENI MWA EPL

DAUDA TV: HIVI NDIVYO ARSENAL ILIVYOSHINDWA KUKWEA KILELENI MWA EPL

460
0
SHARE

Southampton

Club ya Arsenal imeshindwa kukwea kileleni mwa ligi kuu England baada ya kukubali kipigo cha magoli 4-0 kutoka kwa Southampton kwenye mchezo uliochezwa December 26 (Jumamosi) usiku.

Kama The Gunners wangeshinda mchezo huo wangefikisha jumla ya ponti 39 na kuishusha Leicester City kileleni ambayo inaponti 38. Kipigo cha Arsenal dhidi ya Southampton ni habari njema kwa Leicester City ambayo bado inaendelea kuongoza ligi licha ya kuchezea kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa Liverpool.

Mabao ya Leicester City yalikwamishwa wavuni na Cuco Martina dakika ya 19 likiwa ni bao la kwanza, bao la pili likafungwa na Shane Long dakika ya 55 lakini akapika pia bao jingine dakika ya 90 ya mchezo wakati Jose Miguel Fonte yeye alifunga bao la tatu dakika ya 69.

Kipigo hicho kimeendelea kuiacha Arsenal katika nafasi yake ya pili ikiwa na pointi 36 wakati vinara wa ligi hiyo Leicester City wakiwa na pointi 38 kileleni huku Manchester City wakifataia katika nafasi ya tatu kwa pointi zao 35, Tottenham inakamisha top four ikiwa na jumla ya pointi 32.

Angalia viedo ya magoli yote ya Southampton vs Arsenal

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here