Home Dauda TV DAUDA TV: AMIS TAMBWE ANAENDELEA KUWATESA MAGOLIKIPA WA VPL

DAUDA TV: AMIS TAMBWE ANAENDELEA KUWATESA MAGOLIKIPA WA VPL

440
0
SHARE
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la tatu kwa style ya pekee
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la tatu kwa style ya pekee
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la tatu kwa style ya pekee

Tambwe amekuwa habari ya mjini kwa sasa na hii ni baada ya kutupia goli tano kwenye mechi mbili za ligi kuu Tanzania bara.

Tambwe alifunga bao mbili wakati Yanga ikicheza dhidi ya Mbeya City na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa bao 3-0. Bao jingine la Yanga lilifungwa na kiungo mshambuliaji Thaban Kamusoko lakini mtengenezaji wa bao hilo alikuwa ni Tambwe ambaye alipiga pasi ya mwisho kwa mfungaji.

Kwenye mchezo kati ya Yanga dhidi ya Stand United Amis Tambwe alifunga bao bao tatu wakati mchezo wa jana amerudi kambani mara mbili na kufanikiwa kufunga bao tano kwenye mechi mbili.

Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake Mwinyi Haji (nyuma) pamoja na Deus Kaseke
Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake Mwinyi Haji (nyuma) pamoja na Deus Kaseke

Tambwe anamtoa mshambuliaji wa Stand United Elius Maguli kileleni mwa orodha ya wafungaji bora baada ya kufikisha magoli 10 na kumwacha maguli kwa tofauti ya goli moja.

Dauda TV ‘Timu ya Ushindi’ inakupa fursa ya kushuhudia magoli yote yaliyofungwa kwenye mchezo huo pamoja na matukio muhimu yaliyojiri kwenye mchezo huo. Angalia video hapa chini ujionee mwenyewe.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here