Home Kimataifa CURRY AENDELEA NA MWAKA BORA WA AJABU, ATWAA TUZO NYINGINE KUBWA.

CURRY AENDELEA NA MWAKA BORA WA AJABU, ATWAA TUZO NYINGINE KUBWA.

621
0
SHARE

curry

Stephen Curry kawa Stephen Curry. Anaimbwa kuliko mchezaji mwingine yeyote. Anaonekana kupanda kiwango kuliko mchezaji mwingine yeyote. Analeta mchezo mpya ambaye hakuna aliyewahi kufikiri kuwa wachezaji aina ya curry wangeweza kuiteka dunia.

Curry kabadili aina ya mchezo wa NBA au basketball kwa ujumla. Mbinu zake za kushoot mipira hazijawahi kutokea. Ubunifu wake na mbinu zilizokuwa mikononi mwake mi nadra kuzipata. Na sasa anaiteka NBA kwa staili ya kipekee.

Baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji mwenye thamani zaidi katika NBA msimu uliopita, sasa Curry aendelea kuchanja mbuga. Ameshinda tuzo ya vyombo vya habari nchini Marekani inayosimamiwa na Associate Press (AP).

Hii ni tuzo ambayo uhusisha michezo yote nchini Marekani. Curry kashinda mwanamichezo bora wa kiume wa mwaka yaani  (The Associated Press 2015 Male Athlete of the Year.) Amechukua tuzo hii akiwashinda wachezaji Jordan Spieth ambaye ni mchezaji wa gofu na alishinda mataji mawili.

Pia kamtungua Farasi ambaye anafahamika kama American Pharoah. Pharoah alishinda mashindano manne na kuweka rekodi ya kuwa farasi wa kwanza kushinda Grand slam. Pia Pharoah alikuwa farasi wa kwanza kushinda mataji matatu yaani TRIPLE CLOWN tangu mwaka 1978.

Matokeo hayo yalitangazwa Jumamosi ya wiki hii ikihusisha Waharirri wa Marekani na pia waongozaji wa habari wa Marekani pia. Curry anakuwa mchezaji wa nne pekee katika historia ya NBA kushinda tuzo hii kongwe ambayo ina miaka 85. Wachezaji wengine waliowahi kushinda tuzo hii ni  LeBron James, Michael Jordan na Larry Bird.

TIZAMA SAFARI YA CURRY KWENDA KUSHINDA  MVP MSIMU ULIOPITA..

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here