Home Kitaifa AZAM YAIPUMULIA YANGA KILELENI

AZAM YAIPUMULIA YANGA KILELENI

567
0
SHARE
Shomari Kapombe akipongezwa na wachezaji wanzake wa Azam FC baada ya kuifungia timu yao bao la pili
Shomari Kapombe akipongezwa na wachezaji wanzake wa Azam FC baada ya kuifungia timu yao bao la pili
Shomari Kapombe akipongezwa na wachezaji wanzake wa Azam FC baada ya kuifungia timu yao bao la pili

Magoli kutoka kwa Kipre Tchetche na Shomari Kapombe yameipa Azam ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Kipre Tchetche aliifungia Azam bao la kuongoza dakika ya 11 kipindi cha kwanza bao ambalo lilidumu kwa muda wote wa kipindi cha kwanza.

Salum Kanoni (kulia) akichuana na Kipre Tchetche
Salum Kanoni (kulia) akichuana na Kipre Tchetche

Baada ya kupata bao hilo Azam walijikuta wakibanwa vilivyo na Kagera Sugar ambao walimiliki mchezo kwa asilimia nyingi na kutengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kukwamisha mipira wavuni.

Wakati dakika za kipindi cha kwanza zinakaribia kumalizika, Kagera Sugar walipata mkwaju wa penati baada ya beki wa Azam kuunawa mpira kwenye eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo kuamuru lipigwe tuta. Beki wa zamani wa Simba SC Salumu Kanoni akapiga penati hiyo lakini ikaokolewa na mlinda mlango wa Azam FC Aishi Manula.

Shomari Kapombe (kushoto) akimtoka beki wa Kagera Sugar
Shomari Kapombe (kushoto) akimtoka beki wa Kagera Sugar

Kipindi cha pili bado Azam walikuwa kwenye wakati mgumu kwasababu walizidi kubanwa na Kagera Sugar kwa muda mwingi wa kipindi cha pili lakini bado tatizo la kushindwa kuzitumia nafasi zilizopatika kupachika mabao liliendelea kuwaandama.

Dakika ya 78 Shomari Kapombe akazima matumaini ya Kagera Sugar kupata japo pointi moja ugenini baada ya kumzidi mbio beki wa Kagera Sugar Juma Jabu na kutupia mpira kambani kuipa Azam FC bao la pili na la ushindi kwenye mchezo huo.

Kwenye mchezo huo Kagera Sugar watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi nyingi za wazi walizotengeneza baada ya kufanikiwa kuwashika Azam kwa muda mwingi wa mchezo.

Juma Jabu akiondosha mpira kwenye hatari mbele ya Kipre Tchetche
Juma Jabu akiondosha mpira kwenye hatari mbele ya Kipre Tchetche

Azam FC imefikisha pointi 32 pointi moja nyuma ya vinara wa VPL Yanga SC ambao wanapointi 33 wakiwa mbele kwa mchezo mmoja kwani wao wameshacheza michezo 13 hadi sasa.

Kagera Sugar wao bado wapo kwenye nafasi ya 15 wakiwa na pointi tisa nafasi moja mbele ya African Sports ya Tanga ambayo inaburuza mkia ikiwa na pointi saba tu baada ya kushuka dimbani mara 13.

African Sports leo imepata ushindi wake wa pili kwenye msimu huu wa ligi baada ya kuchomoza na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Toto Africans kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here