Home Dauda TV MASHALI AKATA NGEBE ZA CHEKA, AMTEMBEZEA KICHAPO NYUMBANI KWAO MOROGORO

MASHALI AKATA NGEBE ZA CHEKA, AMTEMBEZEA KICHAPO NYUMBANI KWAO MOROGORO

499
0
SHARE
Thomas Mashali (kushoto) na Francis Cheka (kulia) wakisubiri mwamuzi (katikati) amtangaze mshindi: Thomas Mashali aliibuka mshindi wa pambano hilo

Bondia maarufu nchini Thomas Mashali amefanikiwa kumpiga kwa pointi bondia mgumu nchini Francis Cheka kwenye pambano la raundi 10 lililopigwa usiku wa Christmas (December 25, 2015) kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Pambano hilo la uzito wa Kg 77 ambalo lilikuwa si la ubingwa liliwakutanisha wawili hao ili kukata mdomo wa nani mkali kati yao na hatimayeThomas Mashali akafanikiwa kumkalisha Cheka akiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Kwa muda mrefu Cheka amekuwa mgumu kupigwa akiwa Morogoro lakini Mashali amevunja mwiko huo kwa kumchakaza Cheka kwa pointi.

Majaji wamempa Mashari pointi 94, 96 na 97 wakati mwenyeji Cheka amepata pointi 96, 93 na 93.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here