Home Kimataifa DRAYMOND GREEN ANAITAKA ALL STAR, STEPHEN CURRY AENDELEA KUIMBWA NA WARRIORS YAILAMBA...

DRAYMOND GREEN ANAITAKA ALL STAR, STEPHEN CURRY AENDELEA KUIMBWA NA WARRIORS YAILAMBA CLEVELAND NA LEBRON WAKE.

543
0
SHARE

DRAY

Wakati Curry yupo kimya, Warriors huitaji mchezaji mwingine asimame. Msimu uliopita muda mwingi alikuwa anaibuka Klay Thompson lakini msimu ni jina jipya limeibuka sasa na linalotawala vinywa vya mashabiki nalo ni Draymond Green.

Hana tofauti kubwa na mchezaji wa San Antonio Spurs, Kawhi Leonard. Wote wanakaba vyema na pia wameongezeka vyema katika upande wa ushambualiji. Draymond Green anawapa Warriors kitu cha ziada zaidi nacho ni pasi za mwisho.

Draymond Green alifunga pointi 22 na kudaka rebound 15 na pasi 7 akiiongoza Warriiors kuibuka na ushindi wa 83-89. Huu unakuwa ushindi wao wa 32 mfululizo katika uwanja wao wa nyumbani huku ikiwa ni mara yao ya kwanza kwa zaidi ya mwaka mmoja kushindwa kufikisha pointi 100 katika uwanja wa nyumbani.

Mchezaji Stephen Curry aliwapa wasiwasi mashabiki wengi kwa kuhisi ameumia mguu. Curry alipelekwa katika vyumba vya kubadilishia nguo kwa uchunguzi zaidi lakini alirejea na kumaliza na pointi 19, pasi 7 na rebound 7.

Klay Thompson aliongeza pointi 18 na kudaka rebound 6. Wakati Curry ameumia Shaun Livingston aliibuka na kufunga pointi 16. Andre Iguodala alimaliza na ointi 7 lakini ulinzi wake dhidi ya lebron uliamua mchezo kwa kiasi kikubwa.

Lebron James alifunga pointi nyingi zaidi katika mchezo huo 25, na kudaka rebound 9. J.R Smith alifunga pointi 14, Irving ambaye bado anarejea mchezoni akitoka majeruhi alifunga pointi 13. Kevin Love alimaliza na pointi 10 na rebound 18.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here