Home Kimataifa KOBE AENDELEA KUTELEZA NA MASHABIKI, AMKATA CURRY, LEBRON NA DURANT KURA ZA...

KOBE AENDELEA KUTELEZA NA MASHABIKI, AMKATA CURRY, LEBRON NA DURANT KURA ZA KUINGIA ALL STAR.

437
0
SHARE

kobe

Mashabiki wa mchezo wa kikapu duniani kote wameendelea kumuaga Kobe Bryant kwa staili ya aina yake. Ukiachilia mbali katika viwanja tofauti anakoenda, sasa wamehamia katika upigaji kura wa kuchagua wachezaji watakaoshiriki mchezo wa mastaa (NBA ALL STAR GAME)

Mashabiki hawajajali kiwango alichokuwanacho Stephen Curry kwa sasa wala umaarufu wa Lebron na badala yake kura nyingi zimeonekana kwenda kwa Kobe Bryant. Katika matokeo ya kwanza yaliyotoka inaonekana Kobe kawazidi wachezaji wengine kwa kiwango kikubwa cha kura.

Mpaka sasa Bryant ana kura 719,235, akimtangulia kwa mbali Stephen Curry  mwenye pointi (510,202). Kobe pia kapata kura nyingi zaidi ya mara mbili alizopata staa wa Cleveland  LeBron James (357,937). Kobe ana kura nyingi kuzidi kura walizopata Durant  (349,473) na Lebron kwa pamoja.

Kobe Bryant aliyetangaza kustaafu mwishoni mwa msimu yupo katika msimu wake wa 20 na ameshachaguliwa kushiriki jumla ya All Star 17. Ni nyingi zaidi nyuma ya idadi ya Kareem Abdul-Jabbar mwenye 19. Kobe pia ndiye mchezaji aliyefunga pointi nyingi zaidi katika All Star akiwa na jumla ya pointi 280.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here