Home Kitaifa CHEKA,MASHALI, KUMALIZA UBISHI LEO? NI KATIKA PAMBANO LA UBABE VS KISASI

CHEKA,MASHALI, KUMALIZA UBISHI LEO? NI KATIKA PAMBANO LA UBABE VS KISASI

707
0
SHARE
Mabondia wakitunishiana mshuli (kulia) Francis Cheka na (kushoto) ni Thomas Mashali
Mabondia wakitunishiana mshuli (kulia) Francis Cheka na (kushoto) ni Thomas Mashali
Mabondia wakitunishiana mshuli (kulia) Francis Cheka na (kushoto) ni Thomas Mashali

Mabondia Francis Cheka wa Morogoro ambaye ni bingwa wa ngumi za kulipwa duniani wa uzito wa kati (WBF) pamoja na Thomas Mashali wa Dar es Salaam kila mmoja ametamba kumpiga mwenzake katika pambano lisilo la ubingwa litakalounguruma leo December 25, 2015 kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mabondia hao walipima uzito jana maeneo ya Msamvu, Morogoro na mabondia wote walikuwa na uzito wa Kg 77. Fransis Cheka amesema amejiandaa vizuri huku Mashali akisema haogopi kupigana na bondia mwenye jina kubwa.

“Siwezi kusema nitampiga raundi ya ngapi, mdomo unaweza kuzungumza lakini mkono hauwezi kuzungumza”, ametamba Cheka dhidi ya mpinzani wake Mashali.

“Francis Cheka naweza kumpiga vizuri ni bondia wa kawaida sana, halafu sio bondia mwenye profile kubwa sana katika mchezo wa ngumi tofauti na mimi ambaye nimepigana sana kuliko yeye. Mimi nimepigana sana, wakati mimi napigana sijui yeye alikuwa wapi”, amesema Mashali.

Mabondia hao walizikunja kwa mara ya mwisho mwaka 2013 ambapo Cheka alimtembezea kichapo Mashali, je Cheka ataendeleza ubabe kwa Mashari au Mashari atalipa kisasi na kufuta uteja kwa Cheka?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here