Home Kitaifa NDOLANGA HAJAKUBALINA NA ADHABU WALIOPEWA BLATTER, PLATINI, YEYE ALITAKA WAPEWE ADHABU HII…

NDOLANGA HAJAKUBALINA NA ADHABU WALIOPEWA BLATTER, PLATINI, YEYE ALITAKA WAPEWE ADHABU HII…

529
0
SHARE
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), Alhaj Muhidin Ndolanga
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), Alhaj Muhidin Ndolanga
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), Alhaj Muhidin Ndolanga

Kiongozi mkongwe wa soka la Tanzania pamoja na mdau mkubwa wa mchezo huo Alhaj Muhidin Ndolanga ameibuka na kuweka hadharani maoni yake juu ya adhabu iliyotolewa kwa kiongozi wa juu wa shirikisho la soka duniani FIFA pamoja na yule wa Ulaya, hawa si wengine bali ni Sep Blatter pamoja na Michel Platini.

Akitoa maoni yake kuhusu viongozi hao kufungiwa kwa miaka nane kujihusisha na masuala ya soka, Ndolanda ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) amesema adhabu hiyo haiwatoshi viongozi hao kwasababu wamekutwa na hatia na hawajapinga huku akiongeza kwa kusema kuna kiongozi ameshawahi kufungiwa maisha kujihusisha na soka kutokana na  masuala ya kujihusisha na rushwa kama ilivyo kwa Blatter na mwenzake Platini.

Kwa maoni yangu ni kwamba kama mtu ni kiongozi wa mchezo mkubwa kama huu wa mpira wa miguu unatuhumiwa kwamba umefanya kosa, inateuliwa kamati inashughulikia hilo suala, tuhuma zinathibitishwa kwamba ni kweli umefanya wanavyosema ni lazima uadhibiwe. Na adhabu hii maana yake nafikiri pengine watu hawajui, ungeniuliza maoni yangu juu ya adhabu hii kama ni sahihi mimi ningesema adhabu hii si sahihi

Hawa walikuwa wanatakiwa wafungiwe maisha kabisa, kwasababu huko nyuma Mohamed bin Hammam alituhumiwa ana mambo ya kutoa rushwa wala haikujulikana ni kiasi gani akafungiwa maisha sasa hawa wamejulikana kabisa wamepeana dola za kimarekani milioni mbili na wamekubali kwamba wamechukua hiyo pesa na kamati imethibitisha hilo inawafungia miaka nane.

Maana yake kwamba Platini atakapofunguliwa hatoweza kugombea tena urais wa FIFA muda wake utakuwa umepita, watu wanaopita muda wa miaka 75 hawawezi wakagombea uongozi FIFA.

Lakini ile kamati imeboronga huwezi kuwakamata watu na rushwa halafu ukawafungia miaka nane, hii kamati ni ya hovyo kabisa hawawezi kujitetea wale (Blatter na Platini).

Nafikiri watu ambao wanafikiri Blatter alikuwa akitufanyia wema bara la Afrika na wanadhani kufungiwa kwake ndiyo mwisho wa misaada ya FIFA kuja Afrika hawayajui vizuri haya mambo. Blatter hakutufanyia wema sisi, haya mabo yaliamuliwa kwenye mkutano haijalishi kama alikuwa anataka au hataki alikuwa anatakiwa kufanya hivyo.

Hakuna habari kusema sisi tulikuwa tunampenda Blatter na sasa anaondoka itakuaje, yale mambo ambayo tulikuwa tunafanyiwa ni lazima tufanyiwe kwasababu yalikuwa ni maamuzi ya FIFA na siyo mapenzi ya Blatter.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here