Home Kitaifa EL MAAMRY KASEMA MENGI KUHUSU KUFUNGIWA KWA BLATTER NA PLATINI, HIKI NDICHO...

EL MAAMRY KASEMA MENGI KUHUSU KUFUNGIWA KWA BLATTER NA PLATINI, HIKI NDICHO KILICHO MSHTUA

565
0
SHARE
Aliyewahi kuwa mjumbe wa CAF, Said Hamad El Maamry
Aliyewahi kuwa mjumbe wa CAF, Said Hamad El Maamry
Aliyewahi kuwa mjumbe wa CAF, Said Hamad El Maamry

Mdau mkubwa soka nchini Said el Maamry ambaye pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa soka ndani na nje ya Tanzania ameeleza namna alivyopokea taarifa za kufungiwa kwa Blatter na Platini kujihusisha na masuala ya soka kwa muda wa miaka nane.

El Maamry amesema alistushwa na taarifa hizo kutokana na imani kubwa aliyokuwanayo kwa viongozi hao wa soka ambao ni wazoefu na wenye heshima kubwa kwenye historia ya soka ulimwenguni.

Nilipokea kufungiwa kwao kwa mshtuko mkubwa kwasababu sikutegemea kwamba wao Blatter na Platini katika hali waliyokuwa wameutumikia mpira wanaweza kufanya mambo wanayoshutumiwa wameyafanya. Kwasababu Blatter hata Platini wote kwa pamoja siyo watu masikini wakusema watashtuka na pesa hizo tunazoambiwa kwamba wamechukua lakini ulimwengu ndivyo ulivyo mtu unavyo mhisi sivyo alivyo.

Mimi binafsi nilikuwa naimani kubwa na Blatter pamoja na Platini lakini nimeshtushwa sana baada ya wao kukutwa na hatia kwa yale waliyokuwa wakituhumiwa nayo.

Tunachotakiwa kujifunza hapa sisi wengine ambao tumebaki kwenye ulimwengu wa mpira kwamba, mambo yote yanayohusu pesa ni vizuri yakaandikwa ili kutoa wasiwasi kwamba huenda kuna kitu ndani ya pesa ambazo zinatoka bila kuandikwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here