Home Kimataifa MTIZAME SANA KAHWI LEONARD, SPURS HAISHIKIKI….

MTIZAME SANA KAHWI LEONARD, SPURS HAISHIKIKI….

541
0
SHARE

KAHW

Wakati Warriors wanashinda wanavyotaka, huku Spurs San Antonio wanashinda wanavyojisikia. Wanatakata na wanakupa sababu ya kuamini kuwa mshindani mkubwa wa Warriors wala hayupo mbali. Wapo vizuri haswa.

Lakini haya yote lazima yaambatane na mchezaji fulani ama wachezaji fulani. Ukiachana na mchezaji wao mpya Lamarcus Aldridge ambaye bado anajiweka vyema kwenye mfumo wa San Antonio kuna mwokozi mpya. Kawhi Leonard ameendelea pale alipokuwa ameishia msimu uliopita.

Wakati akisifika kwa kuwa mkabaji mzuri kupindukia, sasa ameongeza upande ulio bora sana, ushambuliaji. Anafunga vyema, amechukua majukumu yake mapya ipasavyo na anawaweka Spurs sehemu salama kila kukicha.

Kawhi Leonard alfajiri ya leo alifunga pointi 24 akadaka rebound 6 na kutoa pasi 5 na kuisaidia Spurs kuinyonyoa timu ngumu ya Indiana Pacers kwa jumla ya pointi 109-92. Kazi yake haikuishia hapo tu kwani aliweza kumkaba vyema Paul George na kumfanya afunge pointi chache zaidi msimu huu, pointi 7.

San Antonio sasa ina rekodi ya 24-5 ikiwa ni rekodi yao ya pili kwa ubora ya kuanza msimu vyema katika historia ya klabu hiyo huku pia wakiwa na rekodi ya kutokufungwa nyumbani katika michezo 16.

Tony Parker alifunga pointi 15, Boris Diaw akaongeza pointi 14 huku LaMarcus Aldridge na Patty Mills kila mmoja akifunga pointi 10. David West alifunga pointi 7 ukiwa ni mchezo wake wa kwanza dhidi ya klabu yake hiyo ya zamani tangu aihame msimu huu kuelekea Spurs.

George Hill na Jordan Hill kila mmoja alifunga pointi 15 kwa Indiana Pacers yenye rekodi ya 16-11.

HIGHLIGHTS

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here