Home Ligi EPL Yaya Toure amepondwa kwa perfomance ya jana Vs Arsenal.

Yaya Toure amepondwa kwa perfomance ya jana Vs Arsenal.

435
0
SHARE

yaya

Yaya Toure licha ya kufunga goli pekee la Manchester City kwenye mechi ya jana dhidi ya Arsenal lakini baadhi ya watu wanasema alikuja na majukumu zaidi ya kufunga goli hilo, na majukumu hayo hakuyatimiza.

Jamie Carragher akiongea kwenye uchambuzi na Sky Sports alimponda pia Yaya Toure kwamba harakati zake za dakika 20 za mwisho ilikua ni mipango ilicholewa sana kusaidia timu yake.

Carragher alisema,”Nadhani ni utani kwa mchezaji kama yeye ambae anategemewa sana na club yake, kama tulivyomsikia mtangazaji wa mechi hii hajakosea kabisa kwa kusema Yaya amekua alive dakika 20 za mwisho. Kama alishtuka na kusema ohh, bado tuna nafasi ya kufunga na kuna nafasi chache za kutumia. Sababu kubwa ya Arsenal kushinda leo ni perfomance nzuri ya Ozil ambayo ameipata kutokana na Yaya Toure kutotumia vizuri eneo lake. Ukimzungumzia Yaya Toure ni level ya mchezaji kiongozi kwa Manchester City, kuanzia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo hadi uwanjani, amekua mbinafis na mtu asiyetimiza majukumu yake kwenye mechi hii”.

Hayo ni mawazo ya Jamie Carragher, unadhani kweli Yaya Toure hakutimiza majukumu yake vizuri ndani ya dakika 90 za mchezo? Nipe maoni yako hapa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here