Home Dauda TV DAUDA TV: ARSENAL MWENDO MDUNDO EPL, YAIKALISHA MAN CITY

DAUDA TV: ARSENAL MWENDO MDUNDO EPL, YAIKALISHA MAN CITY

541
0
SHARE

Mangala

Magoli mawili yaliyofungwa na Theo Walcott pamoja na Olivier Giroud yameiwezesha Arsenal kuibuka na pointi tatu kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Manchester United kwenye mchezo uliochezwa usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne mchezo uliomalizika kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa bao 2-1.

Kama kawaida yake ‘King of Assists’ Mesut Ozil alitengeneza mabao yote mawili kabla ya kukwamishwa na wafungaji. Arsenal ilipiga kamba zake zote kipindi cha kwanza. Goli la kwanza likifungwa dakika ya 33 na Walcott wakati Giroud yeye alipiga la pili dakika ya 45.

walcott_ozil

Yaya Toure alifanikiwa kuipatia timu yake bao la kufutia machozi dakika ya 82 kipindi cha pili kwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na beki wa kulia wa timu hiyo Sagna.

Matokeo hayo yanawafanya The Gunners kufikisha pointi 36 ponti mbili nyuma ya vinara wa ligi hiyo Leicester City ambao wanaongoza ligi wakiwa na pointi 38 huku timu zote zikiwa zimecheza michezo 17 hadi sasa. Manchester City bado wataendelea kusalia kwenye nafasi ya tatu wakiwa na pointi zao 32 nyuma ya Arsenal.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here