Home Ligi EPL Man United Kwenye Anguko: Mambo 3 Yaliyosababisha Kipigo cha Jana

Man United Kwenye Anguko: Mambo 3 Yaliyosababisha Kipigo cha Jana

514
0
SHARE

Safari ya Manchester United kucheza bila ushindi jana ilifikia mechi 6, wakati kikosi cha Louis Van Gaal kilipofungwa Old Trafford na moja ya timu zilizokuwa na matokeo mabaya msimu huu Norwich.

Vipigo vya Back-to-back  vya Premier League vimewafanya United watoke ndani ya listi ya timu za Top 4 na hali inazidi kuwa mbaya kwa kocha wao mdachi.

Katika kipigo cha jana kuna vitu vitatu nimejifunza.UMRI (Wachezaji wakubwa zaidi au Wadogo zaidi
)

Wachezaji muhimu wa United wengi wao wameshavuka kilele cha viwango vyao –   Michael Carrick, Bastian Schweinsteiger, Wayne Rooney – na pia wanaochepukia bado hawajafikia kwenye level ya juu ya viwango vyao –  Memphis Depay na Anthony Martial.
Wachezaji wamenunuliwa kwa fedha nyingi na wanautayari mzuri zaidi katika kuimarika kwa viwango vyao – mfano Morgan Schneiderlin na Ander Herrera, jana waliachwa benchi.

 Mashabiki wa United walikuwa wakipiga kelele wakimtaka kocha amuingize Herrera na wakati alipoingia walisimama wote na kumpa heshima ya ‘standing ovation’.
 KAMALI ZA  VAN GAAL

Wayne Rooney ni kiungo wikii, namba 10 kesho, centre forward wiki ijayo.  Marouane Fellaini alisifiwa mno kwankuwa mshambuliaji mzuri na LVG msimu uliopita, lakini sasa kocha huyo anamuona Mbelgiji huyo kama kiungo.
Ashley Young ameshajaribiaa kama beki wa kushoto na wa upande wa kulia, pia ameshajaribiwa kama winga wa upande wa kushoto na wa kulia pia.

Hakuna consistency kwenye uchaguzi wa kikosi. Van Gaal anaonekana ni mcheza kamari asiye na umakini, anayecheza bila mipango akiwa na imani atashinda lotto.
 NAHODHA ASIYE NA SIFA 

Van Gaal alisema msimu uliopita kwamba nahodha ni lazima acheze. Rooney ndio nahodha wake lakini kiwango chake msimu huu kimekuwa mdhoofu mno.

Rooney hawezi kulaumiwa kwa vipigo vitatu vilivyopita – alikuwa majeruhi lakini bado katika mchezo wa jana alikuwa dhaifu, mchezo ambao ulikuwa wa 500 tangu alipoanza kuitumikia United.

United itawabidi wafanye maamuzi nini cha kufanya juu ya mchezaji wao anayelipwa zaidi, je atakuwa miongoni mwa mipango ya muda mrefu, kama yupo atakuwa kwenye nafasi gani. Hawezi kuwa kiongozi wa timu kama hastahili kucheza katika kikosi cha kwanza, soka halipo namna hiyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here