Home Kitaifa HII NDIYO SABABU ILIYOMFANYA TAMBWE KU-DEDICATE HAT-TRICK KWA MTOTO WAKE

HII NDIYO SABABU ILIYOMFANYA TAMBWE KU-DEDICATE HAT-TRICK KWA MTOTO WAKE

797
0
SHARE
Amis Tambwe akishangilia moja ya goli lake alilofunga kwenye mchezo wa leo kati ya Yanga dhidi ya Stand United
Amis Tambwe akishangilia moja ya goli lake alilofunga kwenye mchezo wa leo kati ya Yanga dhidi ya Stand United
Amis Tambwe akishangilia moja ya goli lake alilofunga kwenye mchezo kati ya Yanga dhidi ya Stand United

Mshambuliaji wa Yanga mrundi Amisi Tambwe jana alifanikiwa kufunga magoli matatu (hat-trick) kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara wakati Yanga ikicheza dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Tambwe amei-dedicate hat-trick hiyo moja kwa moja  kwa mtoto wake ambaye yuko na mama yake nchini  Burundi

“Nilizungumza na mtoto wangu kabla ya mchezo wetu dhidi ya Stand United akaniambia tunakutakia ufanye vizuri kwenye mchezo wako. Namshukuru sana mtoto wangu na hii zawadi ya mpira ni ya mtoto wangu na nitampelekea nyumbani”, alisema Tambwe mara baada ya mchezo wa jana kumalizika.

Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe akionesha mpira kwa mashabiki baada ya kukabidhiwa na mwamuzi wa mchezo wa leo Ludovic Charles baada ya Tambwe kufunga bao tatu katika mchezo wa leo
Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe akionesha mpira kwa mashabiki baada ya kukabidhiwa na mwamuzi wa mchezo  Ludovic Charles baada ya Tambwe kufunga bao tatu

“Siyo rahisi kufunga hat-trick hasa kwenye msimu huu ambao ni mgumu kuliko ule uliopita, ni kujituma na kujitoa lakini naamini nitafanya vizuri”.

“Hapa nipo kikazi nikiweka kichwani mambo ya machafuko yanayoendelea nyumbani siwezi kufanikiwa kwenye kazi yangu. Ili nifanikiwe inabidi nisifikirie sana mambo yanayoendelea nyumbani kwasababu nikifiria sana siwezi kufanikiwa na kufanya vizuri na mimi hii ndiyo kazi yangu inayonifanya niishi”.

“Lakini hali ya vita ikizidi kuendelea nitalazimika kuichukua familia yangu na kuihamishia huku ambako mimi nipo”.

Amisi Tambwe akikabidhiwa mpira na mwamuzi Ludovic Charles baada ya mchezaji huyo kufunga magoli matatu kwenye mchezo kati ya Yanga dhidi ya Stand United
Amisi Tambwe akikabidhiwa mpira na mwamuzi Ludovic Charles baada ya mchezaji huyo kufunga magoli matatu kwenye mchezo kati ya Yanga dhidi ya Stand United

Hali ya kisiasa ni tete kwa sasa nchini Burundi wananchi wakiwa wanapinga hatua ya Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunzinza  ambaye anaongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here