Home Ligi BUNDESLIGA FUTURE YA GUADIOLA SASA HADHARANI

FUTURE YA GUADIOLA SASA HADHARANI

533
0
SHARE

Pep-Guardiola

Mustakabali wa kocha Pep Guadiola kuendelea kuifundisha Bayern Munich ama kutoendelea unatarajiwa kuwekwa wazi wiki ijayo mara baada ya mazungumzo na uongozi wa Bayern baada ya kumalizika kwa mchezo wa Bayern Munich na Hannover Jumamosi hii kisha kupisha mapumziko ya baridi ‘winter break’.

Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenige amesema kuwa kama walivyoahidi huko nyuma kwamba kutakua na mazungumzo na kocha huyo, sasa muda ni muafaka kwani watakaa pamoja mara baada ya mchezo wa Hannover jumamosi hii na kujua nini kinafuata.

Mkataba wa Guadiola unaishia mwisho wa msimu huu na tayari taarifa zinasambaa kwamba kocha huyo anaweza kuwa njiani kuelekea ligi kuu nchini England ambapo vilabu vya Manchester United na City vyote vinawinda huduma ya kocha huyo.

Manchester City imekua ikihusishwa zaidi na kumtaka kocha huyo ingawa miezi kadhaa iliyopita kuliibuka tetesi kwamba kocha huyo ana mahaba zaidi na klabu ya Manchester United kutokana na uhuru wa klabu hiyo kwa kocha lakini hasa akihofia tabia ya timu aina ya Manchester City ambazo hukosa uvumilivu na makocha mambo yanapokua tofauti.

Lakini awali huko nyuma aliwahi utaja mji wa London kuwa ni sehemu anayopenda kuishi akiwa nchini England, jiji ambalo zipo timu za Arsenal, Chelsea na Tottenham Hotspur.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here