Home Kimataifa UNAJUA NINI KIMETOKEA KATIKA SERIE A RAUNDI YA 16??UNGANA NAMI…

UNAJUA NINI KIMETOKEA KATIKA SERIE A RAUNDI YA 16??UNGANA NAMI…

638
0
SHARE

SERIE LEO

Mchezo wa jana kati ya SSC Lazio dhidi ya Sampdoria ulihitimisha raundi ya 16 ya Ligi Kuu ya soka nchini Italia maarufu kama Serie A.Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya goli 1-1.

Yapo mambo mengi yaliyotokea katika raundi ya 16 ya Serie A kwa msimu huu.

REKODI HIZO NI ZIPI?

Klabu za Napoli na AS Roma hazijawahi kutoka sare ya bila kufungana tangu mwezi April tarehe 9 mwaka 1995.Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Estadio San San Paolo.Sare hii inakuja baada ya michezo 24 baina ya timu hizo ambayo imezaa magoli 74.

Mara ya mwisho kwa klabu ya As Roma kushinda katika uwanja wa Estadio San Paolo ilikuwa Desemba mwaka 2011 walipopata ushindi wa magoli 3-1.Cha kushangaza katika mchezo wa Napoli na Roma ni kuwa Roma haikupiga shuti lolote lililolenga goli la Napoli kwa dakika zote 90 huku wakigusa mpira mara 5 tu katika boksi la Napoli.

Mara ya mwisho kwa Roma kushindwa kupiga shuti lililolenga goli  ilikuwa ni mwaka 2008 walipocheza na Juventus.

Wakati raundi ya 10 inachezwa,klabu ya Roma ilikuwa ipo mbele kwa pointi 11 mbele ya Juventus.Lakini mpaka sasa ikiwa ni raundi 16,Roma wapo mbele kwa pointi 1 tu mbele ya Juventus.Katika kipindi cha wiki 5 zilizopita,Juventus imefanikiwa kukusanya pointi 18 huku Roma  ikikusanya pointi 6 tu.

 

Mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain ameshindwa kufikia rekodi ya Diego Maradona kwa kufunga magoli katika mechi 9 mfululizo ndani ya uwanja wa Estadio San Paolo.Ila mpaka sasa Higuain anaongoza kwa magoli katika Serie A akiwa na magoli 14.

Ushindi wa Juventus wa magoli 3-1 mbele ya Fiorentina umeifanya klabu ya Juventus kufikisha ushindi wa sita mfulululizo katika Serie A.Klabu ya Fiorentina imeendelea kuwa kibonde kwa Juventus kwa kupoteza michezo 5 iliyopita katika mji wa Turin huku mara ya mwisho kupata pointi ilikuwa mwaka 2010 walipolazimisha sare ya 1-1 na pia ushindi wa magoli 3-2 mwaka 2008.

Wakati Juventus wakizidi kuweka rekodi  katika Serie A,klabu ya Inter Milan chini ya Kocha Roberto Manchini nayo imeingia katika rekodi za Serie A katika raundi ya 16.Ushindi dhidi ya Udinese wa magoli 4-0 umeifanya klabu ya Inter Milan kukusanya jumla ya pointi 17 za ugenini  katika Serie A msimu huu.

Idadi hiyo ya pointi ni kubwa kuliko zile zilizokusanywa na Inter ya Jose Mourinho ya msimu wa 2009/10.

Lakini kingine kwa upande wa Inter Milan ni kuwa kwa mara ya kwanza Inter inafunga zaidi ya goli 1 katika kipindi cha kwanza katika Serie A msimu huu.Lakini zaidi ya hapo ni mara ya kwanza kuona wachezaji wa Inter Stefan Jovetic na Mauro Icardi wakifunga kwa pamoja katika Serie A.

Idara ya ulinzi ya Inter Milan inayoongozwa na Miranda na Jeison Murillo imeruhusu magoli 9 tu mpaka sasa katika raundi  16.Mara ya mwisho kwa Inter kuruhusu magoli machache katika raundi 16 ni msimu wa mwaka 2007 waliporuhusu magoli 8 tu katika michezo 16.

Klabu ya Hellas Verona haijawahi kushinda katika michezo 26 iliyopita dhidi ya AC Milan  ingawa imefanikiwa  kupata sare katika michezo 11.Mchezo wa Ac Milan dhidi ya Hellas Verona  ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1ndio mchezaji uliozaa kadi nyingi kuliko mchezo wowote ule wa Serie A msimu huu.Mchezo huo umeshuhudia kadi 9 za njano na kadi moja nyekundu.

Kadi  nyekundu katika mchezo huo ilikwenda kwa kiungo mkabaji wa Ac Milan Nigel De Jong na kuwa kadi nyekundu ya kwanza kwake kwa msimu huu.

Mshambuliaji  wa klabu ya Hellas Verona Luca Toni  anazidi kuionesha umwamba klabu ya Milan baada ya kuifungia Hellas Verona goli la kusawazisha na kumfanya kufikisha magoli 9 katika michezo 17 dhidi ya Ac Milan yakiwepo magoli 4 katika michezo minne iliyopita.

Milan wanapata sare ya pili dhidi ya timu zinazoshika mkia ambazo ni Carpi na Hellas Verona.

Klabu ya Sampdoria haijawahi kuifunga klabu ya Lazio nyumbani na ugenini kwa miaka 5 sasa tangu mwaka 2010 walipopata ushindi wa magoli 2-0 mbele ya Lazio.Kabla ya hapo Sampdoria wamepoteza michezo 6 kati ya 7 huku wakiambulia  sare ya 1-1 mwaka 2013 mwezi Novemba.

Klabu ya Lazio haijashinda mchezo wowote wa Serie A tangu wafanye hivyo mwezi Oktoba walipoifunga Torino magoli 3-0.Hali hiyo pia ipo kwa Sampdoria chini ya kocha Vicenzo Montella ambaye kwa mara ya kwanza sare dhidi ya Lazio ndio matokeo mazuri aliyopata tangu aichukue Sampdoria toka kwa Walter Zenga.

Montella amepoteza michezo 3 mpaka sasa na kuambaulia sare 1 dhidi ya Lazio.

Na klabu ya Atalanta ndio klabu yenye nidhamu mbovu kuliko timuz ote zilizo katika Ligi 5 bora barani Ulaya.Mpaka sasa Atalanta ina kadi 9 nyekundu zikiwa nyingi kuliko timu zote za Ligi mbalimbali barani Ulaya

Highlights

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here