Home Kimataifa Madrid vs AS Roma: Je Ronaldo na Wenzake Watavunja Mwiko wa Kutozitoa...

Madrid vs AS Roma: Je Ronaldo na Wenzake Watavunja Mwiko wa Kutozitoa Timu za Italia Uliodumu kwa Miaka 29

684
0
SHARE

REAL MADRID wameondolewa kwenye michuano ya kombe la Copa Del Rey wiki iliyopita na juzi wameendelea kufanya vibya kwenye ligi baada ya kukubali kipigo cha 3 msimu huu mbele ya Villareal – jambo ambalo limezidisha presha kwa kocha, Rafa Benitez.IMG_1427-0.jpg

Na Je inawezekana pia wakawa wanaelekea nje ya michuano ya ulaya pia? Historia inatoa ishara kwamba hiyo inaweza kutoka.

Wababe hawa wa kihispania walipangwa na AS Roma katika droo iliyofanyika jana ya hatua ya 16 bora – Madrid hawajawahi kuitoa timu yoyote ya Italia katika hatua ya mtoano katika kipindi cha miaka 29 iliyopita.

02_15115608_4a31e6_2605181aKlabu hiyo yenye mafanikio zaidi katika michuano ya barani ulaya wameondolewa kwenye michuano hii na AC Milan, Torino, Juventus wakawatoa mara 4 na hata AS Roma pia imewahi kuwaondoa kwenye michuano hii.

Mara ya mwisho kwa Madrid kuitoa timu ya italia kwenye michuano hii ya ulaya ilikuwa mwaka 1987 vs Napoli.

REKODI YA REAL MADRID VS TIMU ZA ITALIA

1988-89 European Cup semi-final

Real Madrid 1 AC Milan 1

AC Milan 5 Real Madrid 0

1989-90 Europen Cup second round

AC Milan 2 Real Madrid 0

Real Madrid 1 AC Milan 0

1991-92 Uefa Cup semi-final

Real Madrid 2 Torino 1

Torino 2 Real Madrid 0

1995-96 Champions League quarter-final

Real Madrid 1 Juventus 0

Juventus 2 Real Madrid 0

2002-03 Champions League semi-final

Real Madrid 2 Juventus 1

Juventus 3 Real Madrid 1

2004-05 Champions League last 16

Real Madrid 1 Juventus 0

Juventus 2 Real Madrid 0 (Aet)

2007-08 Champions League last 16

Roma 2 Real Madrid 1

Real Madrid 1 Roma 2

2014-15 Champions League semi-final

Juventus 2 Real Madrid 1

Real Madrid 1 Juventus 1

04_15115608_92d50c_2605183a
Pedrag Mijatovic akiifungia Real Madrid goli la ushindi dhidi ya Juventus katika fainali ya UCL 1998 – Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Madrid kupata kuweza kuitoa au kushinda mechi ya hatua isiyo ya makundi dhidi ya timu ya Kiitaliano tangu mwaka 1966

Hata hivyo Real Madrid walifanikiwa kuifunga Juventus kwenye fainali ya Champions League mwaka 1998.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here