Home Kimataifa UNATAKA KUJUA NINI KIMETOKEA KWENYE VYUMBA VYA KUBADILISHIA NGUO BAADA YA TP...

UNATAKA KUJUA NINI KIMETOKEA KWENYE VYUMBA VYA KUBADILISHIA NGUO BAADA YA TP MAZEMBE KUPOTEZA MCHEZO WA ROBO FAINALI KLABU BINGWA DUNIA?….HUYU HAPA MBWANA SAMATTA

642
0
SHARE

Samatta-JPN 6

Na Shaffih Dauda, Osaka, Japan

December 13 ulipigwa mchezo wa klabu bingwa duniani hatua ya robo fainali kati ya Sanfrecce Hiroshima dhidi ya TP Mazembe mchezo ambao ulimalizika kwa TP Mazembe kupigwa magoli 3-0 na kushindwa kusonga mbele kwenye mashindano hayo.

Kama kawaida nimemtafuta nyota wa TP Mazembe na Tanzania Mbwana Samatta nikapiganae story nikitaka kujua nini kimepelekea timu yake ishindwe kufurukuta mbele ya wajapan kinyume na matarajio ya watu wengi huku nikitaka kujua pia hali ilikuaje kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kikosi cha TP Mazembe kushindwa kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

“Imekuwa tofauti na matarajio ya wengi, sisi tulikuwa tunakaa sana mipira na mwalimu aliliona hilo na kutuambia wakati wa mapumziko. Sehemu pekee ambayo sisi tungeweza kupita kuirahisi zaidi ilikuwa ni pembeni, katikati jamaa walikuwa wamesimamisha mabeki watatu ambao ni total defenders kwahiyo ilikuwa vigumu kupita katikati na njia pekee ilibidi tupite pembeni lakini mwisho wa siku mambo yakawa tofauti, amesema Samatta striker wa TP Mazembe na timu ya taifa ya Tanzania.

“Baada ya mchezo kumalizika wachezaji walikuwa wamenyong’onyea sana kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwasababu kitu ambacho tulikuwa tunakitarajia kimekuwa tofauti”.

“Wakati tunaingia tulikuwa na furaha kwasababu tuliwaangalia wapinzani wetu kwenye mechi yao ya kwanza tukawa na confidence jamaa hawa tunaweza tukawafunga lakini tumekutana na kitu tofauti kwahiyo kidogo imekuwa ngumu na watu wamenyong’onyea”.

Siku ya Jumatano TP Mazembe itacheza na Clab America ya nchini Mexico katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tano na wa sita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here