Home Kimataifa EXCLUSIVE INTERVIEW: SAMATTA AMTAJA ANAYEMHOFIA TUZO ZA MCHEZAJI BORA AFRIKA

EXCLUSIVE INTERVIEW: SAMATTA AMTAJA ANAYEMHOFIA TUZO ZA MCHEZAJI BORA AFRIKA

688
0
SHARE
Mwana Samatta akiwa Osaka, Japan kwenye michuano ya kombe la vilabu bingwa duniani
Mwana Samatta akiwa Osaka, Japan kwenye michuano ya kombe la vilabu bingwa duniani
Mbwana Samatta akiwa Osaka, Japan kwenye michuano ya kombe la vilabu bingwa duniani

Na Shaffih Dauda, Osaka, Japan

Baada ya CUF kutangaza majina ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezji bora wa Afrika mwaka 2015 kwa upande wa wachezaji wanaocheza vilabu vya Afrika, amechomoza mtanzania Mbwana Aly Samatta na kuingia kwenye top 3 ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo. Wengine ni Baghdad Boundjah (Algeria/ Etoile du Sahel) na Robert Kidiaba (DRC/ TP Mazembe).

Mtandao huu umepata fursa ya kuzungumza na Mbwana Samatta hapa Osaka, Japan kuhusiana na yeye kuingia kwenye hatua ya fainali kuwania tuzo ya mchezaji bora Afrika na anajisikiaje kufika hatu hiyo na anaona ananafasi gani katika tuzo hizo.

Shaffihdauda.co.tz: Kwanza nikupongeze kwa kufanikiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watatu waliofanikiwa kupita kuwania tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika, unajisikiaje kuwa miongoni mwa wachezaji watatu waliofika hatua ya fainali?

Samatta: Asante sana Shaffih, mimi najisikia vizuri sana kwanza ukiondoa mimi binafsi, vilevile nakuwa proud na taifa langu ni kama nalitangaza kwani watu wanapojua kama Samatta ni mtanzania wanaanza kuangalia kama Tanzania imetoa kipaji ambacho kimeweza kuwa bora Afrika basi inawezekana kuna vipaji vingine vingi. Kwahiyo inatangaza Tanzania na soka letu na kuweza kupata wengine ambao wanaweza kufanikiwa zaidi ya hapa.

Shaffihdauda.co.tz: Mwanzoni kabisa, ulitegemea utakuwa miongoni mwa haya majina matatu yaliyoingia hatua ya fainali?

Samatta: Taarifa nimeipokea kwa furaha kwasababu ni achievement kama mchezaji binafsi lakini hili suala nililitegemea lakini halikuwa 100% kutokana na mwaka jinsi ulivyoisha mafaniko niliyoyapata kama mchezaji, kama timu ni suala ambalo nilitegemea kwa asilimia flani. Si kwamba limetokea kama bahati hapana, na hii yote imetokana na timu yangu kuchukua ubingwa na mimi mwenyewe kuwa katika wachezaji ambao wamefanya vizuri katika mwaka huu.

Shaffihdauda.co.tz: Ni mchezaji yupi unayemuhofia zaidi kati ya Baghdad Boundjah na Robert Kidiaba?

Samatta: Kwa mimi nafikiri wote wananafasi kwasababu mshambuliaji wa Etoile du Sahel ameisaidia timu yake kuchukua ubingwa wa Confederation Cup, zadi nafikiri ni Kidiaba kwasababu ana-mudamrefu akiwa anacheza soka la Afrika na hajawahi kuingia katika hatua kama hii na ni legend kwenye soka la Afrika kwahiyo ananipa mashaka nadhani labda anaweza kuwa mshindi lakini hatujui kwasababu tupo kwenye tatu bora lolote linaweza kutokea, wote tuliopo tatu bora ni bora kwa mwaka huu kwahiyo tusubiri tuone.

Shaffihdauda.co.tz: Taarifa za kuwa na Robert Kidiaba miongoni mwa wachezaji watatu wanao wania tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika itakuwa imewaongezea motivation kiasi gani kuelekea  kwenye mechi yenu dhidi ya Club America?

Samatta: Kiasi chake inaleta chachu kidogo ya kuweza kurudi kwenye ari kwa haraka na kuweza kufanya vizuri japo imekuja katika wakati ambao ari ya timu ni tofauti. Timu imekuwa haina morali kubwa, lakinini nadhani  tusubiri tutakapokuwa kwenye mchezo ari itakuwaje. Lakini kwa mimi binafsi nadhani inaamsha ari kwamba naweza nikafanya kitu, naweza nikacheza mechi yangu ya mwisho vizuri na nikafanya vizuri nikalinda heshima ya timu, heshima ya Samatta na heshima ya Tanzania pamoja na Afrika kwa ujumla.

Hapa chini unaweza kusikiliza interview ya Samatta mwanzo mwisho akipiga story na Shaffih Dauda wakiwa Japan kwenye michuano ya FIFA Club World Cup.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here